Wednesday 19 September 2018



Pokea hizi nyimbo mpya kutoka kwa Chidi Benz, Chemical, Beka Flavor, Snura na Dully Sykes!

Serious enius - Chidi Benz > https://mkito.com/song/21803
Tilalila - Chemical > https://mkito.com/song/21802
Siwezi - Beka Flavor > https://mkito.com/song/21693
Kadamshi - Dully Sykes > https://mkito.com/song/21667

Ngoma mpya kutoka kwa Chidi Benz, Chemical, Beka Flavor, Snura na Dully Sykes!


Kampuni hiyo maarufu ya kutengeza vinywaji vilaini ipo kwenye mazungumzo na Kampuni ya kutengeneza bangi, Aurora Cannabis ili kutengeneza kinywaji hicho
-
Inaelezwa kuwa lengo kuu la Kinywaji hicho kitakachotengenezwa na bangi aina ya cannabidiol litakuwa ni kupunguza maumivu(kutumika kama dawa) na si kulewesha
-
Aidha, Kampuni hiyo bado haijazungumza hadharani mpango huo lakini imekiri kwamba inafuatilia kwa karibu matukio katika sekta ya vinywaji vyenye bangi
-
Cannabidiol ni moja ya viungo vinavyopatikana ndani ya bangi na kinaweza kusaidia kupunguza kuvimba, maumivu na kuganda kwa misuli

KAMPUNI YA VINYWAJI YA COCACOLA YAJIPANGA KUTENGENEZA KINYWAJI CHENYE BANGI


-
Michezo miwili ya mapema ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya imemalizika ambapo Barcelona na Inter Milan zimeibuka na ushindi
-
Katika mchezo wa Barcelona na PSV Eindhoven, Mchezaji Lionel Messi ameibuka nyota wa mchezo kwa kufunga magoli matatu(hat-trick) huku goli moja likifungwa na Ousmane Dembele
-
Katika Mchezo wa Inter Milan dhidi ya Tottenham, goli la Spurs limefungwa na Christian Eriksen huku magoli ya Inter yakifungwa na Mauro Icardi na Matias Vecino

BARCELONA YANG'ARA, TOTTENHAM YALA KICHAPO

Tuesday 18 September 2018


Bondia Anthony Joshua AJ wa Uingereza ametangaza kuwa kamwe hatadharau pambano lake la jumamosi dhidi ya Alexander 'Sasha' Povektin wa Urusi litakalopigwa jumamosi ijayo Septemba 22 katika uwanja wa Wembley mjini London.
Katika pamabano hilo, AJ anatarajiwa kutetea mikanda yake mitatu ya ubingwa wa WBO, IBF na WBA huku akiwa na shinikio kubwa la kulinda rekodi ya kutowahi kupigwa katika mapambano yote 21 aliyowahi kushiriki tangu aanze masumbwi.
Povektin mwenye rekodi ya kupoteza pambano moja tu kati ya 35 aliyowahi kushiriki amekutana na mpinzani wake kwenye mkutano wa kutambulisha pambano hilo jana.

Bondia Anthony Joshua asema hatodharau pambano la jumamosi


Msimu mpya wa ligi ya klabu bingwa ulaya wa mwaka 2018-2019 unaanza rasmi usiku wa leo ambapo jumla ya mechi nane kati ya timu kutoka makundi A, B, C na D zitashindana katika michezo ya mzunguko wa kwanza.
Miongoni mwa mechi zitakazopigwa kesho, PSG ya Ufaransa itakuwa na kibarua kizito ugenini dhidi ya Liverpool ya Uingereza, nayo Inter Milan itakuwa nyumbani nchini Italia kuikatibisha Tottenham ya Uingereza.
Barcelona ya Hisapania itakuwa nyumbani kucheza na PSV ya Uholanzi, Monaco ya Ufaranza ikicheza na Atletico Madrid ya Hispania.
Nayo Crvena Zvezda ya Serbia itacheza dhidi ya Napoli ya Italia, Schalke ya Ujerumani dhidi ya Porto ya Ureno, Lokomotiv Moscow ya Urusi itakuwa ugenini nchini Uturuki kucheza na Galatasaray, na Club Brugge ya Ubeligiji itaikaribisha Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya: Msimu mpya kuanza leo

Monday 17 September 2018


Mshambuliaji wa @simbasctanzania Meddie Kagere ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti wa #TanzaniaPremierLeague 2018/2019.
Kagere amewashinda Joseph Mahundi (Azam FC) na Ompar Mponda (Kagera Sugar) alioingia nao fainali.
.

Meddy Kagere atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.


The African Prince Nandy amesema kuwa ikifika 2020 ataachana rasmi na mziki na kuanza kufanya biashara kwani ndio ndoto yake toka zamani.
.
.
Akihojiwa katika kipindi cha Leo Tena Nandy ameeleza kuwa aliweka malengo baada ya miaka kadhaa aweze kuachana na kazi ya muziki.
.
.
"Mimi ndoto zangu ni kuwa mfanyabiashara mkubwa sana na hata wakati naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo baada ya miaka mitano niache muziki na niendeleze biashara zangu na mpaka sasa nimeitumia miaka miwili (2016 na 2017) na mwaka 2020 ndiyo nitaacha muziki, Na sio kwamba nitakuwa sitoi ngoma hapana nitakuwa natoa sema kwa mwaka hata mara moja ha show naweza kuwa nafanya mara moja kwa mwaka ili nipate muda mzuri wa kusimamia biashara zangu" @officialnandy .
.

Nandy atangaza kuacha mziki ikifika 2020.



Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’ amesema licha ya kuwa bado ana hofu, kesho anarejea Uganda kutoka Marekani alikoenda kupatiwa matibabu, amesema wasiwasi alionao hata Waganda milioni 44 pia wanao na Uganda ndiko iliko familia yake na watu wake hivyo lazima arudi.

Bobi Wine kurejea Uganda


Hatimaye Cristiano Ronaldo afanikiwa kuifungia Juventus goli lake la kwanza baada ya kufunga magoli mawili na kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Sassuolo
-
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33, alicheza mechi 3 bila kufunga goli na ilimchukua dakika 5 tu za kipindi cha pili kuweza kupata goli hilo la kwanza
-
Goli lake la kwanza limekuja ikiwa ni shuti lake la 28 la kujaribu kupata goli katika michezo minne kwa ajili ya Juventus sawa ya michezo na mashuti aliyochukua msimu uliopita akiwa Real Madrid ili kupata goli lake la kwanza
-
Aidha, goli lake la leo la pili ni goli la kihistoria kwani ni goli lake la 400 katika michuano yote ya ligi akiwa amecheza michezo 517. Magoli 311 alifunga akiwa Real Madrid, 84 akiwa Manchester United na 3 akiwa Sporting Lisbon

Ronaldo ageuka 'lulu' Juventus


Kimetua nchini humo leo na kupiga eneo la Guangdong ambalo ni eneo lenye watu wengi zaidi huku kikitishia kuleta madhara makubwa Hong Kong na Macau
-
Kinasafiri maili 170 kwa saa na kwa mujibu wa shirika la kutoa tahadhari za vimbunga la Marekani mwendokasi huo ni mara mbili ya Kimbunga Florence kinachotishia pwani ya Marekani
-
Aidha, kwenye pwani ya China vinu viwili ya Nyuklia, Yangjiang na Taishan vimeonekana kuwepo katika njia ya Kimbunga hicho lakini Mamlaka katika kinu cha Yangjiang imesema ipo tayari na imejizatiti kujilinda
-
Kwa upande mwingine, daraja refu zaidi duniani linalokatisha baharini lenye urefu wa maili 34 lililogharimu dola za Kimarekani Bilioni 20 lipo hatarini kutokana na kukatiza kwenye Bahari ya Kusini ya China ambapo Kimbunga hicho kinapita
-
Daraja hilo linalounganisha Hong Kong, Macau na Zhuhai lilitengenezwa kukaa miaka 120, kuhimili upepo wa kasi ya maili 120 kwa saa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa Kipimo cha tetemeko richa 8

KIMBUNGA CHAIPIGA CHINA BAADA YA KUUA TAKRIBANI 50 UFILIPINO


Kupitia msemaji wake Ofono Opondo yautaka Muunganiko huo wa Ulaya kutatua matatizo yake kwanza na kuacha kuingilia masuala ya bara la Afrika
-
Yasema haitakubali Umoja wa Ulaya kuishurutisha kufanya masuala yasiyouhusu na kuwa Uganda ina mifumo yake ya kujitawala
-
Aidha, imesema kuwa uhasama wake na EU ni kutokana na kushindwa kuidhinisha ndoa za jinsia moja na uhusiano wake na nchi ya China
-
Kauli hizo zinakuja ikiwa ni baada ya EU kuitaka Serikali ya Museveni kuheshimu haki, demokrasia na Mihimili mingine ya Serikali ikiwemo Bunge

UGANDA YAITAKA EU KUACHA KUINGILIA MASUALA YA AFRIKA

Sunday 16 September 2018


Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake Kikatiba kuwaachia huru wafungwa 2,000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu
-
Miongoni mwa wafungwa hao ni Mwanamuziki, Kizito Mihigo aliyekuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Kiongozi wa Upinzani, Victoire Ingabire aliyekuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 tangu 2010
-
Bi. Ingabire alirudi kutoka jela nchini Uholanzi mwaka 2010 ili kushiriki katika uchaguzi wa urais lakini alikamatwa na kuzuiliwa kuwania urais
-
Aidha, ni Hutu aliyekuwa akihoji ni kwanini makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini humo ya mwaka 1994 hayakuhusisha watu wa kabila la Hut

RWANDA: ALIYEKUWA KIONGOZI WA UPINZANI ATOKA GEREZANI KWA MSAMAHA WA RAIS



Klabu ya Manchester United imefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Watford katika mchezo wa mzunguko wa 5 wa Ligi Kuu soka nchini humo

Kwa matokeo hayo Manchester United inashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 9 huku Watford ikishika nafasi ya 4 ikiwa na alama 12
-
Kuangalia msimamo mzima wa Ligi hiyo, angalia picha ya pili

Msimamo ligi kuu England mechi za jana

Saturday 15 September 2018


-


Sonia Fanuel mkazi wa Nyegezi jijini Mwanza anashikuliwa na Polisi kwa kukutwa na funguo bandia 53 za vitasa pamoja na 101 za Makufuli
-
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jonathan Shanna amesema msichana huyo alikamatwa Septemba 13 saa 1:45 jioni mtaa wa Rose Kata ya Nyegezi
-
Shanna alieleza kuwa Sonia alikamatwa baada ya wasichana wawili, Esther Isaack na Ruth Sumari kukuta milango ya vyumba vyao imefunguliwa huku mtuhumiwa akiwa amejibanza ukutani
-
Amesema Wasichana hao walipokagua mali zao ndani walibaini Tsh. 160,000 zimeibwa na nguo zenye thamani ya Tsh. 200,000

MSICHANA WA MIAKA 20 AKAMATWA NA FUNGUO BANDIA 154

Friday 14 September 2018


Jeshi la Polisi linamshikilia Askofu Franco Mulakkal wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Kaskazini mwa Jimbo la Punjab nchini India anayetuhumiwa kwa ubakaji.
-
Anatuhumiwa kufanya matukio hayo katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016
-
Watawa walifanya mgomo kwa siku kadhaa wakishinikiza kukamatwa kwake. Mgomo huo ulijumuisha makundi ya Wanaharakati na Watetezi wa haki za Wanawake

ASKOFU ANAYETUHUMIWA KUMBAKA MTAWA AKAMATWA


Maafisa Usalama wa Uganda wazuia jaribio la mamlaka za Kenya la kutaka kupandisha bendera ya nchi yao katika Kisiwa hicho kinachobishaniwa
-
Waganda wameshusha bendera hiyo iliyopandishwa na Wakenya na kutoa onyo la kuwataka wasirudie kitendo hicho walichokiita ni chokochoko
-
Serikali ya Kenya na Uganda zimekuwa kwenye mgogoro kuhusu umiliki wa kisiwa hicho kilichopo ndani ya Ziwa Victoria tangu mwaka 2004

UGANDA NA KENYA 'ZATUNISHIANA MISULI' KUPANDISHA BENDERA KISIWA CHA MIGINGO

Thursday 13 September 2018


University College London ni cha 18. Kwa kuangazia sifa za vyuo vikuu miongoni mwa waajiri, Cambridge na Oxford ndivyo vinavyoongoza, lakini kwa jumla vyuo vikuu vya Uingereza vilishuka katika ushirikiano na waajiri na viwango vya kuajiriwa kwa wanafunzi wao.
Kuimarika kwa China kunadhihirishwa na kuorodheshwa kwa Tsinghua University nafasi ya tisa na University of Peking nafasi ya 20.

Kati ya vyuo vikuu 500 vilivyoorodheshwa, 102 vinatoka bara Asia, 144 kutoka Ulaya Magharibi. Marekani ina vyuo vikuu 83, ambapo 13 kati ya vyuo hivyo vimo katika orodha ya 30 bora. Afrika kuna vyuo vikuu 10.
Chuo hicho kikuu cha Nairobi ndicho pekee kutoka Afrika Mashariki ingawa kimeshuka kutoka nambari tano Afrika mwaka 2018, mwaka ambao kulikuwa na vyuo vikuu 11 vya Afrika katika vyuo vikuu 500 bora duniani kwenye orodha hiyo.
Vyuo Vikuu vinavyopendwa na waajiri Afrika 2019
  1. University of Cape Town, Afrika Kusini
  2. The American University in Cairo, Misri
  3. University of Witwatersrand, Afrika Kusini
  4. Cairo University, Misri
  5. Ain Shams University, Misri
  6. Stellenbosch University, Afrika Kusini
  7. University of Johannesburg, Afrika Kusini
  8. University of Kwazulu-Natal, Afrika Kusini
  9. University of Nairobi, Kenya
  10. University of Pretoria, Afrika Kusini
Chuo kikuu cha Alexandria cha Misri ndicho kilichotupwa nje katika orodha ya mwaka huu baada ya kuwa nambari nane Afrika mwaka uliopita.
Chuo kikuu cha Cape Town ambacho kinaongoza Afrika katika orodha ya jumla kinashikilia nafasi ya 101-110, na hakuna chuo kingine cha Afrika hadi baada ya vyuo mia ambapo ndipo unapata chuo kikuu cha Kimarekani cha Cairo na Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Afrika Kusini katika nafasi ya 201-250.
Chuo Kikuu cha Nairobi kinashikilia nafasi ya 301-500. Mwaka jana, kilikuwa katika nafasi ya 251-300 kwa jumla.
Mwaka 2017, Afrika ilikuwa na vyuo vikuu vinne pekee, wakati huo orodha hiyo kwa jumla ikishirikisha vyuo vikuu 300 duniani. Mwaka 2017 walishirikisha vyuo 494 na mwaka huu vyuo 497.


Hivi ndio vyuo vinavyopendwa sana na waajiri



"Wakati unasema chanini, wenzako wanasema watapata lini"
Msemo huu umejidhihirisha leo kupitia ukurasa wa mchezaji wa kimataifa kutoka Tanzania anayekipiga KRC Genk nchini Ubelgiji , Mbwana Ali Samata ameandika kuwa ndoto yake kubwa kwa sasa ni kumiliki ndege binafsi (Private Jet)
.
.
"Ndoto za kumiliki private jet zimeanza baada ya kupiga picha hii 🤨 sio kila ndoto inaweza kutimia ila, acha vita ianze😡," ameandika @samagoal77
.
.
Mbwana Samata ni mmoja wa nyota wa mpira mwenye utajiri mkubwa na hiyo ni kutokana na juhudi zake katika mpira.
.

Samata atamani kununua 'Private Jet'


Hatua hii ni matunda ya makubaliano ya amani yaliyosainiwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed na Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki mwezi Julai 2018
-
Ethiopia imeahidi kuanza kuviondoa vikosi vyake katika mpaka wake na Eritrea
-
Mataifa hayo yaliingia kwenye mgogoro uliosababisha vita kati yao kuanzia mwaka 1998-2000. Vita hiyo ilisababisha baadhi ya familia kutengana

MPAKA WA ETHIOPIA NA ERITREA WAFUNGULIWA TENA BAADA YA MIAKA 20 -



Ex Babymama wa msanii @wizkidayo,Binta Diallo amehairisha kupeleka jarada la kesi mahakamani linalohusu kutotoa matunzo kwa mtoto wao Junior.


Binta Diallo amehairisha kesi hiyo kutokana na kuombwa na watu wa karibu wa msanii huyo kutokana na kuharibu utaratibu wa kazi za msanii.
.
.
Hivi karibuni @wizkidayo aliandika kupitia ukurasa wake wa Tweeter kama atajenga shule pale malipo mazuri yatakayotoka katika brand take mpya ya Starboy.
.
. "So, I listened and accepted that deal and gave him a chance to do the right thing. That was 7 months ago and since then his lawyers keep telling my lawyers that they have not been able to reach their client or his management team. more receipts on the way,"

Wikid nusura apelekwe mahakamani kisa matunzo ya mtoto



The 2018 American Music Awards nominations (show airs on Oct. 9th):
.
.
• Artist of The Year = Drake
= Imagine Dragons
= Post Malone
= Ed Sheeran
= Taylor Swift
...................................................
• Best Pop/Rock Album = Drake - Scorpion
= Ed Sheeran - Divide
= Taylor Swift - Reputation
...................................................
• Best Pop/Rock Song = Camila Cabello (ft. Young Thug) - Havana
= Drake - God’s Plan
= Ed Sheeran - Perfect
...................................................
• Best Male Pop/Rock Artist = Drake
= Post Malone
= Ed Sheeran
...................................................
• Best Female Pop/Rock Artist = Camila Cabello
= Cardi B
= Taylor Swift
...................................................
• Best Rap/Hip-Hop Album = Drake - Scorpion
= Lil Uzi Vert - Luv Is Rage 2
= Post Malone - beerbongs & bentleys
...................................................
• Best Rap/Hop-Hop Song = Cardi B - Bodak Yellow
= Drake - God’s Plan
= Post Malone (ft. 21 Savage) - Rockstar
...................................................
• Best Rap/Hip-Hop Artist
= Cardi B
= Drake
= Post Malone
...................................................
• Best Collaboration = Camila Cabello (ft. Young Thug) - Havana
= Post Malone (ft. 21 Savage) - Rockstar
= Bruno Mars (ft. Cardi B) - Finesse
= Bebe Rexha & Florida Georgia Line - Meant To Be
= Zedd, Maren Morris & Grey - The Middle
...................................................
• Best Music Video
= Camila Cabello (ft. Young Thug) - Havana
= Cardi B - Bodak Yellow
= Drake - God’s Plan
...................................................
• Best New Artist = Camila Cabello
= Cardi B
= Khalid
= Dua Lipa
= XXXTENTACION

The 2018 American Music Awards nominations

Wednesday 12 September 2018

Mchoraji katuni kutoka nchini Australia
  
 
 
 
 
 
 
 
 
                                                                                                                              
                                       Mchoraji katuni kutoka nchini Australia Mark Knight,ameshutumiwa na kitendo cha ubaguzi kutoka katika katuni aliyoichapisha kupitia ukurasa wake wa Tweeter ikimuonesha mcheza Tenisi namba moja duniani Selena William akiwa analalamika katika katuni hiyo huku ikiwaonyesha refa wa Us Open 2018 akimwambia mshindi wa mashindano hayo upande wa wanawake "Can you just let her win"

Kibonzo cha Selena Williams chaibua 'Utata'


Timu ya taifa ya Hispania imeendeleza makali yake kwenye michuano ya ligi ya mataifa ya Ulaya kwa kupata ushindi mnono wa magoli 6-0 ikiwa nyumani jana usiku dhidi ya Croatia kwenye mjini Elche.
Magoli ya Hispania yalifungwa na Samuel Niguez, Marco Asensio, Rodrigo, Sergio Ramos, Isco na jingine moja likiwa ni la kujifunga wenyewe Croatia kupitia Lovre Kalinic.
Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Hispania, kwani katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi walishinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Uingereza.
Katika mechi zingine zilizopigwa jana, Ubeligiji ilishinda kwa magoli 3-0 ilipocheza dhidi ya Iceland, ikifunga kupitia Romelo Lukaku aliyefunga mawili na Eden Hazard aliyefunga moja kwa njia ya Penati.

Hispania yashinda kwa magoli 6-0 dhidi ya Croatia

Tuesday 11 September 2018


Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo aongoza mamia ya waombolezaji kuupokea mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Kofi Annan uliowasili nchini humo ukitokea Jijini Geneva nchini Uswisi
-
Annan aliyewahi kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel(2001), alifariki Agosti 18 mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi
-
Annan aliongoza Umoja wa Mataifa kuanzia Januari 1997 hadi Desemba 2006
-
Aidha, aliwasili mkoani Mbeya(Tanzania) mwaka 2011 na kuitembelea taasisi ya ARI UYOLE inayojihusisha na masuala ya uboreshaji wa kilimo na utafiti katika nchi za Afrika

MWILI WA KOFI ANNAN WAWASILI JIJINI ACCRA UKITOKEA USWISI


Aliyekuwa mume wa mwanamuziki Tiwa Savage kupitia ukurasa wake wa Instagram aeleza juu ya mahusiano mapya na ya siri kati ya Baby Mama wake wa zamani Tiwa Savage na Wizkid.
.
.
Licha ya kuachana Teebillz ameonekana kutopendezwa na kinachoendelea baina ya wawili hao na kumtaka Wizkid kuacha Mara moja kwani Tiwa Savage ni mkubwa kwake kiumri.
.
.
Hata hivyo Teebillz amedai kuwa kitendo hicho ni njia moja wapo ya Wizkid kumvunjia heshima kama mtu aliyemsaidia kutoka kimziki akishirikiana na Banky W.
.
. "Whether you like it or not Ayo is my lil bro and he knows not to cross me on blood gang.

We don’t play that shit on 400 blocks! That’s my lil Nigga and is Big Hommie Sauce kid aka Sinzu guaranteed me on the lil homie even though he’s my blood and Mr Capable Banky W is my blood.

I’m just saying this to the general public that tend to come at me on some disrespectful Shit!

For your information! Thank you Titi for respecting me! your opinion on her and my lil bro Wizzy is bullshit! Don Jazzy! Jazzy! Will never allow that! WizKid they fuck Tiwa? I trusted you fam?

He will never allow that! Tiwa gets mad at me on my own P but she will never put me down like that, She better be fvking with Femi Otedola, Aliko Dangote, Or Mr Adeleke Aka Baba Olowo.

If you are not in that category then FUCK YOU and at the the end of the day my hustle will match on with my responsibilities in my kids names but 4real on Jamil.

Tiwa will never disrespect me like That!!! FuCK your opinion. tiwa savage wizkidayo keep giving us that fire.

Congratulations blood wizkidayo on The NIKE thanks for putting Naija On the Map. Blessings,"
.
.

Teebillz athibitisha mahusiano ya Tiwa Savage na Wizkid



Kazi mpya kutoka katika kundi la weusi inaitwa Swagiree,Itazame Hapa.

WEUSI - SWAGIRE (Official Music Video)

Monday 10 September 2018

Young Killer - Secreto
        Download

Young Killer - Secreto mp3 download


Mwanadada Serena Williams ametozwa faini ya fedha pauni za kiingereza 13,156 kutokana na makosa matatu tofauti aliyoyafanya kwenye mechi ya fainali ya michuano ya tennis ya Marekani uliopigwa siku ya jumamosi.
Kosa la kwanza ilikuwa ni kumtolea maneno ya dhihaka mwamuzi, kosa la pili kuzungumza mara kwa mara na mwalimu wake akiwa mchezoni na kosa la tatu ikiwa ni kuvunja kwa hasira raketi yake ya kuchezea.
Ikumbukwe kuwa kwenye mechi hiyo ya fainali kwa upande wa wanawake, Serena alifungwa na Naomi Osaka kutoka Japan, faini yake hiyo aliilipa kwa lazima kwa fedha hizo kukatwa kwenye malipo ya zawadi yake ya mshindi wa pili zipatazo pauni milioni 1.43.

Serena Williams apigwa faini kwa utovu wa nidhamu


Katika mechi ya fainali kwa upande wa wanaume iliyomalizika asubuhi hii, ya michuano ya US-Open, Novak Djokovic wa Serbia amepata ushindi wa seti 6-3, 7-6 na 6-3 dhidi ya Martin Del Potro wa Argentina.
Huu unakuwa ni ubingwa wa tatu kwa Djokovic kwenye michuano ya US-Open na anaifikia rekodi ya Peter Sampras aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo kwa wanaume.
Lakini kwa idadi ya mataji makubwa ya tennis, ubingwa huu unakuwa ni wa 14 kwa Djokovic na sasa.

Djokovic ubingwa wa US-Open wanaume



Usiku wa kuamkia leo Tanzania kupitia bondia wake Hassan Mwakinyo amemtandika vibaya Muingereza Sam Eggington kwa Technical Knockout round ya pili kwenye mashindano ya uzito wa kati ya WBO.

Mwakinyo amemuangushia kipigo Eggington kabla refarii hajaingilia kati kumuokoa. Kipigo alichopewa kilimfanya ashindwe kusimama wakati refa akitangaza mshindi. Hata kocha wake alipomuuliza unaona, alijibu "sioni kitu". Yani alipigwa hadi akashindwa kuona sawasawa. .
.

Hassan Mwakinyo Bondia aliyeishangaza Dunia



Drake na Meek Mill walikua ni kati ya watu wenye tofauti kubwa na hata watu kutabiri kuwa hawatokuja kupatana kamwe.
Ila hii imekua tofauti baada ya wawili hao kupatana Live mbele ya kadamnasi ya watu waliohudhuria Show.

Drake na Meek Mill wapatana kwenye 'show'



Mkurugenzi na muandaaji wa mashindano ya kumsaka miss Tanzania @basillamwanukuzi amewajibu wale wote wanaobeza zawadi ya gari aliyopatiwa Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth.
.
.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa watu waliokuwepo waliiona zawadi hiyo lakini kuna watu waliopanga kuchafua mashindano hayo na kuedit zawadi hiyo ili waonekane kama matapeli.
.
.
"Wanalazimisha tufanane......🤣🤣
Watu wazima ovyoo. Kuedit na kusambaza hakuondoi ukweli kua you were not serious. At presenting Miss Lake zone prize.
Pongezi kwa The Look company Limited 👏👏👏👏👏," ameandika Basilla.

Basilla: Wanaobeza zawadi ya gari ya Miss Tanzania ni 'Watu wazima Hovyo'



Kampuni kubwa ya kuuza na kutengeneza filamu kwa mara ya kwanza imeamua kuuza filamu iitwayo "Lions Heart" kutoka nchini Nigeria kupitia mtandao wake wa
#netflix.
.
.
Filamu hiyo ambayo ipo chini ya mwanadada Genieveve Nnaji imeoneshwa kwa Mara ya kwanza kupitia #TorontoInternationalFilmFestival.
.
.
Hii ni filamu ya aina yake iliyobeba vionjo vya komedi ndani yake wapo mastaa mbalimbali ambao ni #GenevieveNnaji, #NkemOwoh, #PeteEdochie and #OnyekaOnwenu.

Filamu kutoka Nigeria kuuzwa Netflix