Sunday 29 October 2017

Polisi amuua mzazi mwenzake akiwa lindoni


BABATI, MANYARA
 Jeshi la Polisi linamshikilia Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU), Cosmas James anayetuhumiwa kumuua mzazi mwenzake kwa kumpiga risasi nne. .

Inadaiwa chanzo cha mauaji hayo ni mzozo ulitokea baada ya Regina Daniel(23) kumfuata Askari huyo aliyekuwa lindoni kumdai fedha za matumizi ya Mtoto.

Askari huyo alitumia silaha aliyokuwa nayo lindoni aina ya SMG mali ya Jeshi la Polisi. Na mara baada ya tukio hilo Askari huyo aliitelekeza silaha lindoni na kwenda kujisalimisha polisi.
.

Aidha, Askari waliokwenda eneo la tukio waliokota maganda matatu ya risasi na waliichukua silaha hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Longinus Tibishubwamu amesema mtuhumiwa yupo mahabusu kwa mahojiano kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa pia mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mji wa Babati ya Mrara.

0 comments:

Post a Comment