Showing posts with label Kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Kitaifa. Show all posts

Saturday, 15 September 2018


-


Sonia Fanuel mkazi wa Nyegezi jijini Mwanza anashikuliwa na Polisi kwa kukutwa na funguo bandia 53 za vitasa pamoja na 101 za Makufuli
-
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jonathan Shanna amesema msichana huyo alikamatwa Septemba 13 saa 1:45 jioni mtaa wa Rose Kata ya Nyegezi
-
Shanna alieleza kuwa Sonia alikamatwa baada ya wasichana wawili, Esther Isaack na Ruth Sumari kukuta milango ya vyumba vyao imefunguliwa huku mtuhumiwa akiwa amejibanza ukutani
-
Amesema Wasichana hao walipokagua mali zao ndani walibaini Tsh. 160,000 zimeibwa na nguo zenye thamani ya Tsh. 200,000

MSICHANA WA MIAKA 20 AKAMATWA NA FUNGUO BANDIA 154

Thursday, 6 September 2018



Kijana huyo ambaye ni mgonjwa wa akili alifanyiwa upasuaji huo katika hospitali teule ya Missenye, Mugana na kukutwa pia na viberiti vya gesi, mfuko, vitambaa na ganda la limao

Dkt. Eliud Nyonyi aliyeshiriki kumfanyia upasuaji mgonjwa huyo, Eliud Novart(25) amesema baada ya vitu hivyo kutolewa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri
 

Mganga Mkuu wa Missenye, Dkt. Hamis Abdallah alisema mgonjwa alifikishwa katika Hospitali ya Mugana baada ya kupatiwa rufaa na Hospitali ya Nyakahanga, wilayani Karagwe

Gumzo: Akutwa na Viberiti na vitambaa tumboni

Thursday, 30 August 2018


NA ISDORY NJAVIKE
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage ameitaka
Bodi mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) kushikana na
serikali kuijenga Tanzania itakayokuwa na uchumi wa kati, shirikishi
na viwanda ifikapo mwaka 2025.

Akizundua Bodi mpya  ya TPSF jijini Dar es Salaam, Waziri Mwijage
ameiambia bodi mpya kuwa imepewa jukumu kubwa na sekta binafsi
iliwafanye kazi kwa bidii na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa
Tanzania ikiwemo kuoengoza mapato ya serikali, ajira na kuweka misingi
mizuri kwa ustawi wa sekta hiyo.
"Tumefanya mabadiliko katika bodi hii ya TPSF na mnatakiwa kujuwa jukumu kubwa ambalo mmepewa ni jukumu la kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika kuhakikisha  maongeza mapato nchini yatakayo tokanna na kazi mnazofanya," alisema Waziri Mwijage
Uzinduzi huo wa Bodi mpya ulitanguliwa na uchaguzi ambao Bw. Salum
Shamte alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya TPSF na Bi. Angelina Ngalula
kuwa Makamu Mwenyekiti. Bw.Shamte amechukua nafasi ya Dkt. Reginald
Mengi ambaye muda wake umemalizika.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya, Bw. Shamte mbali ya kuwashukuru
wajumbe wote kwa kumchangua kuwa mwenyekiti, amesema sekta binafsi
lazima itoe mchango mkubwa katika kujenga Tanzania mpya kiuchumi.

Wajumbe waliochanguliwa kwenye bodi hiyo ni Bw. Subhash Patel, Dkt.
Charles Kimei, Fatma Kange, Bw. Dhrur Ashtosh Jog, Bw. Sylivestry
Koka, Bw. Peter Shayo, Bw. Octavian Mshiu,Bw.Abdulsamad Abdulrahim,
Bi. Jacquiline Mkindi na Bw. Sanjay Rughani.
Mwisho.

Waziri Mwijage azindua Bodi Mpya ya TPSF

Wednesday, 29 August 2018


Mkurugenzi wa fedha na Mipango katika hospitali ya Rufaa Bugando, Mtawa Suzan Bathlomeo amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani

Mtawa huyo alijirusha muda mfupi baada ya kutoka kusali misa ya saa 12:00 asubuhi, leo Jumanne Agosti 28, 2018

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jonathan Shana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema taarifa kamili itatolewa na Polisi hapo baadaye
.

TANZIA-Mtawa ajirusha ghorofani

Sunday, 26 August 2018



Rais Magufuli amemtuma Rais mstaafu wa awamu ya 4, Jakaya Kikwete kumuwakilisha kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa

Ataambatana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula na Mwenyekiti chama cha UDP, John Cheyo

Emmerson Mnangagwa alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika Julai 30 mwaka huu

Mnangagwa alimshinda mgombea wa upinzani kupitia chama cha Movement for Democratic Change(MDC), ndugu Nelson Chamisa

Katika uchaguzi huo Mnangagwa kupitia chama kikongwe cha ZANU-PF alipata asilimia 50.8 ya kura zote huku Nelson Chamisa akipata asilimia 44.3 ya kura zote

Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumuwakilisha JPM Zimbabwe

Saturday, 14 July 2018



Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama, akiwa katika mbuga ya Serengeti alikokuja kwaajili ya utalii na familia yake

Inaelezwa kuwa hii ni mara ya pili kwa Obama kuja nchini, ambapo mara ya kwanza ilifanya hivyo mnamo Julai 2013 akiwa bado madarakani

Obama pamoja na familia yake waliripotiwa kuingia nchini kimya kimya siku chache zilizopita kwaajili ya mapumziko na utalii

Obama,Michelle ndani ya Serengeti

Monday, 11 June 2018








MAGAZETI YA LEO JUMATATU 11/6/2018

Sunday, 10 June 2018






MAGAZETI YA LEO JUMAPILI 10/6/2018

Friday, 8 June 2018











MAGAZETI YA LEO IJUMAA 8.6.2018

Thursday, 7 June 2018












MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 7/6/2018

Wednesday, 6 June 2018











MAGAZETI YA LEO JUMATANO 6/6/2018

Tuesday, 5 June 2018







MAGAZETI YA LEO JUMANNE 5.6.2018