Showing posts with label Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kimataifa. Show all posts

Monday, 17 September 2018



Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’ amesema licha ya kuwa bado ana hofu, kesho anarejea Uganda kutoka Marekani alikoenda kupatiwa matibabu, amesema wasiwasi alionao hata Waganda milioni 44 pia wanao na Uganda ndiko iliko familia yake na watu wake hivyo lazima arudi.

Bobi Wine kurejea Uganda


Kimetua nchini humo leo na kupiga eneo la Guangdong ambalo ni eneo lenye watu wengi zaidi huku kikitishia kuleta madhara makubwa Hong Kong na Macau
-
Kinasafiri maili 170 kwa saa na kwa mujibu wa shirika la kutoa tahadhari za vimbunga la Marekani mwendokasi huo ni mara mbili ya Kimbunga Florence kinachotishia pwani ya Marekani
-
Aidha, kwenye pwani ya China vinu viwili ya Nyuklia, Yangjiang na Taishan vimeonekana kuwepo katika njia ya Kimbunga hicho lakini Mamlaka katika kinu cha Yangjiang imesema ipo tayari na imejizatiti kujilinda
-
Kwa upande mwingine, daraja refu zaidi duniani linalokatisha baharini lenye urefu wa maili 34 lililogharimu dola za Kimarekani Bilioni 20 lipo hatarini kutokana na kukatiza kwenye Bahari ya Kusini ya China ambapo Kimbunga hicho kinapita
-
Daraja hilo linalounganisha Hong Kong, Macau na Zhuhai lilitengenezwa kukaa miaka 120, kuhimili upepo wa kasi ya maili 120 kwa saa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa Kipimo cha tetemeko richa 8

KIMBUNGA CHAIPIGA CHINA BAADA YA KUUA TAKRIBANI 50 UFILIPINO


Kupitia msemaji wake Ofono Opondo yautaka Muunganiko huo wa Ulaya kutatua matatizo yake kwanza na kuacha kuingilia masuala ya bara la Afrika
-
Yasema haitakubali Umoja wa Ulaya kuishurutisha kufanya masuala yasiyouhusu na kuwa Uganda ina mifumo yake ya kujitawala
-
Aidha, imesema kuwa uhasama wake na EU ni kutokana na kushindwa kuidhinisha ndoa za jinsia moja na uhusiano wake na nchi ya China
-
Kauli hizo zinakuja ikiwa ni baada ya EU kuitaka Serikali ya Museveni kuheshimu haki, demokrasia na Mihimili mingine ya Serikali ikiwemo Bunge

UGANDA YAITAKA EU KUACHA KUINGILIA MASUALA YA AFRIKA

Sunday, 16 September 2018


Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake Kikatiba kuwaachia huru wafungwa 2,000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu
-
Miongoni mwa wafungwa hao ni Mwanamuziki, Kizito Mihigo aliyekuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Kiongozi wa Upinzani, Victoire Ingabire aliyekuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 tangu 2010
-
Bi. Ingabire alirudi kutoka jela nchini Uholanzi mwaka 2010 ili kushiriki katika uchaguzi wa urais lakini alikamatwa na kuzuiliwa kuwania urais
-
Aidha, ni Hutu aliyekuwa akihoji ni kwanini makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini humo ya mwaka 1994 hayakuhusisha watu wa kabila la Hut

RWANDA: ALIYEKUWA KIONGOZI WA UPINZANI ATOKA GEREZANI KWA MSAMAHA WA RAIS

Friday, 14 September 2018


Jeshi la Polisi linamshikilia Askofu Franco Mulakkal wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Kaskazini mwa Jimbo la Punjab nchini India anayetuhumiwa kwa ubakaji.
-
Anatuhumiwa kufanya matukio hayo katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016
-
Watawa walifanya mgomo kwa siku kadhaa wakishinikiza kukamatwa kwake. Mgomo huo ulijumuisha makundi ya Wanaharakati na Watetezi wa haki za Wanawake

ASKOFU ANAYETUHUMIWA KUMBAKA MTAWA AKAMATWA


Maafisa Usalama wa Uganda wazuia jaribio la mamlaka za Kenya la kutaka kupandisha bendera ya nchi yao katika Kisiwa hicho kinachobishaniwa
-
Waganda wameshusha bendera hiyo iliyopandishwa na Wakenya na kutoa onyo la kuwataka wasirudie kitendo hicho walichokiita ni chokochoko
-
Serikali ya Kenya na Uganda zimekuwa kwenye mgogoro kuhusu umiliki wa kisiwa hicho kilichopo ndani ya Ziwa Victoria tangu mwaka 2004

UGANDA NA KENYA 'ZATUNISHIANA MISULI' KUPANDISHA BENDERA KISIWA CHA MIGINGO

Thursday, 13 September 2018


University College London ni cha 18. Kwa kuangazia sifa za vyuo vikuu miongoni mwa waajiri, Cambridge na Oxford ndivyo vinavyoongoza, lakini kwa jumla vyuo vikuu vya Uingereza vilishuka katika ushirikiano na waajiri na viwango vya kuajiriwa kwa wanafunzi wao.
Kuimarika kwa China kunadhihirishwa na kuorodheshwa kwa Tsinghua University nafasi ya tisa na University of Peking nafasi ya 20.

Kati ya vyuo vikuu 500 vilivyoorodheshwa, 102 vinatoka bara Asia, 144 kutoka Ulaya Magharibi. Marekani ina vyuo vikuu 83, ambapo 13 kati ya vyuo hivyo vimo katika orodha ya 30 bora. Afrika kuna vyuo vikuu 10.
Chuo hicho kikuu cha Nairobi ndicho pekee kutoka Afrika Mashariki ingawa kimeshuka kutoka nambari tano Afrika mwaka 2018, mwaka ambao kulikuwa na vyuo vikuu 11 vya Afrika katika vyuo vikuu 500 bora duniani kwenye orodha hiyo.
Vyuo Vikuu vinavyopendwa na waajiri Afrika 2019
  1. University of Cape Town, Afrika Kusini
  2. The American University in Cairo, Misri
  3. University of Witwatersrand, Afrika Kusini
  4. Cairo University, Misri
  5. Ain Shams University, Misri
  6. Stellenbosch University, Afrika Kusini
  7. University of Johannesburg, Afrika Kusini
  8. University of Kwazulu-Natal, Afrika Kusini
  9. University of Nairobi, Kenya
  10. University of Pretoria, Afrika Kusini
Chuo kikuu cha Alexandria cha Misri ndicho kilichotupwa nje katika orodha ya mwaka huu baada ya kuwa nambari nane Afrika mwaka uliopita.
Chuo kikuu cha Cape Town ambacho kinaongoza Afrika katika orodha ya jumla kinashikilia nafasi ya 101-110, na hakuna chuo kingine cha Afrika hadi baada ya vyuo mia ambapo ndipo unapata chuo kikuu cha Kimarekani cha Cairo na Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Afrika Kusini katika nafasi ya 201-250.
Chuo Kikuu cha Nairobi kinashikilia nafasi ya 301-500. Mwaka jana, kilikuwa katika nafasi ya 251-300 kwa jumla.
Mwaka 2017, Afrika ilikuwa na vyuo vikuu vinne pekee, wakati huo orodha hiyo kwa jumla ikishirikisha vyuo vikuu 300 duniani. Mwaka 2017 walishirikisha vyuo 494 na mwaka huu vyuo 497.


Hivi ndio vyuo vinavyopendwa sana na waajiri


Hatua hii ni matunda ya makubaliano ya amani yaliyosainiwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed na Rais wa Eritrea, Isaias Afwerki mwezi Julai 2018
-
Ethiopia imeahidi kuanza kuviondoa vikosi vyake katika mpaka wake na Eritrea
-
Mataifa hayo yaliingia kwenye mgogoro uliosababisha vita kati yao kuanzia mwaka 1998-2000. Vita hiyo ilisababisha baadhi ya familia kutengana

MPAKA WA ETHIOPIA NA ERITREA WAFUNGULIWA TENA BAADA YA MIAKA 20 -

Tuesday, 11 September 2018


Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo aongoza mamia ya waombolezaji kuupokea mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Kofi Annan uliowasili nchini humo ukitokea Jijini Geneva nchini Uswisi
-
Annan aliyewahi kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel(2001), alifariki Agosti 18 mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi
-
Annan aliongoza Umoja wa Mataifa kuanzia Januari 1997 hadi Desemba 2006
-
Aidha, aliwasili mkoani Mbeya(Tanzania) mwaka 2011 na kuitembelea taasisi ya ARI UYOLE inayojihusisha na masuala ya uboreshaji wa kilimo na utafiti katika nchi za Afrika

MWILI WA KOFI ANNAN WAWASILI JIJINI ACCRA UKITOKEA USWISI

Saturday, 18 August 2018

  •  
    Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Kofi Annan amefariki dunia akiwa na miaka 80
    -
    Mwanadiplomasia huyo amefariki asubuhi ya leo nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi
    -
    Kutokana na umahiri wake Kofi Annan alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Desemba 1996. Na alianza kazi rasmi Januari 1, 1997
    -
    Mwaka 2001 alichaguliwa kwa mara ya pili kuuongoza tena Umoja wa Mataifa. Oktoba 12, 2001 alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel
    -
    Annan alianza kutumikia nafasi mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa(UN) tangu mwaka 1974 ingawa aliacha kazi na kurudi kuiongoza Kampuni ya Utalii nchini mwake
    -
    Mwaka 1976 alirudi tena kwenye ulingo wa siasa za kimataifa na safari yake ndani ya Umoja wa Mataifa ikaanza rasmi
    -
    Kofi Atta Annan alizaliwa Aprili 8, 1938 nchini Ghana

Koffi Anan Afariki Dunia

Saturday, 14 July 2018



Kampuni ya Johnson & Johnson imeamriwa na Baraza la Mahakama kulipa dola bilioni 4.7 (takribani Tsh. Trilioni 10.7) kama fidia na faini kwa wanawake 22 waliodai kuwa bidhaa za kampuni hiyo zimewasababishia saratani ya ovari

Katika kesi hiyo iliyodumu wiki 6, wanawake hao na familia zao wamesema kuwa wamepata saratani ya ovari baada ya kutumia poda ya Johnsons na baadhi ya bidhaa zake

Mawakili wa familia hizo wamedai kuwa kampuni hiyo ilikuwa inatambua kuwa bidhaa yao ya poda ya talc ilikuwa na madini mabaya ya 'asbestos' tangu mwaka 1970 lakini ilikosa kuwaonya watumiaji kuhusu athari

Hata hivyo, Kampuni hiyo ilikana tuhuma hizo na walisisitiza kwamba bidhaa hizo hazileti saratani. Nakuongeza kuwa imesikitishwa sana na ina mpango wa kukata rufaa

Uamuzi huo unakuja wakati ambapo kampuni hiyo kubwa ya dawa ikipambana na kesi 9,000 zinazohusisha bidhaa yake maarufu ya poda

Aidha, Mtaalumu wa mambo ya Afya, James Gallagher amedai kuwa kumekuwa na wasiwasi kwa miaka kadhaa kwamba kutumia poda yenye madini ya talc au talcum, hasa kwenye viungo vya uzazi, inaweza kuongeza hatari ya saratani ya ovari lakini ushahidi haujakamilika

Kampuni ya Johnson yapigwa faini

Friday, 13 July 2018



Kijana mmoja achapwa viboko 80 kwa kosa la kunywa pombe alilotenda akiwa na miaka 14

Aidha kijana huyo alitenda kosa hilo miaka 10 iliyopita na mpaka sasa haieleweki ni kwanini adhabu yake ilichelewa kutekelezwa

Shirika la Kimataifa la Amnesty limelaani adhabu hiyo iliyotekelezwa kwenye Mji ulio Mashariki mwa Jimbo la Kashmir

Ikumbukwe kuwa mwaka 2014, watu 6 walihukumiwa kwenda jela na viboko 91 baada ya kukutwa wakiuchezea wimbo wa Pharrel Williams.

Aidha, mambo mengine yanayoweza kusababisha uchapwe viboko nchini Iran ni pamoja na uzinzi, kubusu hadharani, wizi, vitendo vinavyohusiana na mapenzi ya jinsia moja.

Achapwa viboko 80 kwa kunywa pombe

Tuesday, 10 July 2018



Waziri wa Mambo ya Nje, Boris Johnson ametangaza kujiuzulu wakati nchi hiyo ikiwa kwenye mgogoro uliozuka katika utekelezaji wa mpango wa kujiondoa kutoka katika uanachama wa Jumuiya ya Ulaya 'BREXIT'

Boris anakuwa Waziri wa pili kujiuzulu ndani ya saa chache baada ya Waziri aliyekuwa akishughulikia mpango wa BREXIT, David Davis kujiuzulu

Mawaziri hawa wanajiuzulu wakati ambao Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Theresa May anajiandaa kulihutubia Bunge kuhusu mpango wake mpya juu ya BREXIT

Aidha, ofisi ya Waziri Mkuu imemshukuru bwana Boris na kuongeza kuwa mrithi wake atatangazwa haraka

Waziri wa Mambo ya Nje Uingereza ajiuzuru rasmi



Mtoto(Duduzane Zuma) wa Rais wa zamani, Jacob Zuma ameshitakiwa kwa makosa ya rushwa katika Mahakama ya biashara mjini Johannesburg.

Duduzane Zuma(34) anadaiwa kuwa sehemu ya waliojaribu kumuhonga Naibu Waziri wa Fedha ili kumshawishi achukue nafasi muhimu za juu kwenye Serikali. Mashitaka hayo pia yanahusishwa na familia maarufu ya Gupta

Hata hivyo Duduzane pamoja na Familia ya Gupta wamekana kuhusika na mashitaka hayo

Mwaka 2015, Naibu Waziri wa Fedha, Mcebisi Jonas alidai kupewa ofa ya nafasi ya Uwaziri wa Fedha na hongo ya 600 milioni rand(takirbani Tsh. Bilioni 100) wakati akiwa kwenye kikao na Duduzane, mfanyabishara Fana Hlongwane na Ajay Gupta

Aidha, Duduzane ambaye anaishi Dubai alirejea nchini humo ili kuhudhuria mazishi ya Kaka yake ndipo akakamatwa na hati yake ya kusafiria kuchukuliwa

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 24, 2019 na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana

Mtoto wa Zuma ashtakiwa kwa Rushwa

Monday, 9 July 2018


Serikali yatoa amri mpya ya kuwafukukuza kazi takribani watumishi wa umma 18,500
Amri hiyo itawagusa Askari wa Jeshi la Polisi, Wanajeshi na watumishi wa taasisi za elimu

Kwa mujibu wa taarifa rasmi aliyotolewa katika gazeti la Serikali imeeleza kuwa watumishi 18,632 idadi inayojumuisha maafisa wa polisi 8,998

Hatua hizi zinachukuliwa ikiwa ni katika kusafisa Serikali baada ya taifa hilo kunusurika katika mapinduzi yaliyopangwa na kukwama mnamo mwezi Julai 2016

Uturuki kuwachukulia hatua wasaliti wa taifa

Thursday, 5 July 2018



Wakati wanandoa huko Wisconsin waliendesha kumkaribisha mtoto wao sio mama tu alikuwa na usiku uliokumbwa na visanga bali baba pia alishiriki kwa njia ambayo hakuwa ameitarajia.

Kujifungua kwake April Neubauer, hakukuwa rahisi kwa sababu alikumbwa na tatizo linalofahamika kama pre-eclampsia, na mpigo wa juu wa damu, hali iliyosababisha akimbizwe chumba cha dharura cha upasuaji.

Wakati mtoto Rosalie alizaliwa tarehe Juni 26, mama yake April alikumbwa na tatizo lingine ndipo akapelekwa kwa matibabu zaidi kabla ya hata kumshika mtoto wake.

Kwa sababu ya hilo mtoto Rosalie ambaye alikuwa na uzani wa kilo 3.6 akakabidhiwa baba yake Maxamilllian. "Muuguzi akaja na msichana wangu mrembo , tukaenda chumba cha watoto, nikaketi na kuvua shati langu ili nimkumbatie mtoto," aliiambia BBC.

Muuguzi akasema kuwa walihitaj kumpa mtoto maziwa ya unga kwanza. "Kisha muuguzi akauliza kama nitaweza kutoa titi langu nimnyonyeshe. Na mimi nikiwa mtu ambaye anapenda kujaribu mambo, nikasema mbona nisifanye hivyo"

Muuguzi akaunganisha mrija ambao ulikuwa umeunganishwa na sirinji iliyokuwa na maziwa ya unga kwa kifua chake Maxamillian.

BABA AMNYONYESHA MWANAYE BAADA YA MKEWE KUSHINDWA.

Wednesday, 4 July 2018



Mwanamke mmoja amelazwa katika hospitali ya Leratong baada ya kukutwa hai katika jokofu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti

Mfanyakazi katika chumba hicho aligundua bado mwanamke huyo anapumua wakati alipofika kuutizama mwili na kutayarisha nyaraka kumhusu

Mwanamke huyo alifikishwa katika chumba hicho baada ya madaktari kusema amefariki kutokana na kutoonesha dalili zozote za uhai kufuatia ajali ya barabarani aliyoipata

Familia ya mwanamke huyo imesema wamepata mshtuko mkubwa na wana wasiwasi kuhusu mkasa huo hivyo wanahitaji ufafanuzi ni vipi makosa hayo yanaweza kutokea

Akutwa hai kwenye chumba cha kuhifadhia maiti

Thursday, 28 June 2018



Taarifa ya furaha iliwafikia Wakenya kuwa Mwanamama tajiri duniani, Oprah Winfrey ataikanyaga ardhi yao kwa mara ya kwanza.

#Oprah alitajwa kuwepo kwenye msafara wa ugeni wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ambaye ametajwa kuwasili nchini Kenya Julai 16 mwaka huu kwa shughuli mbili: Kuitembelea ikulu ya Kenya ambapo atatunukiwa tuzo ya heshima pia baadae atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Uzinduzi wa NGO ya dada yake, Dr. Auma Obama itakayo fanyika kijijini kwao, K'Ogelo.

Sasa taarifa rasmi kutoka kituo cha Televisheni cha CNN zimeripoti kuwa, Oprah Winfrey hatokuwepo na taarifa zile za awali zilikuwa ni uzushi mtupu
"But it's not accurate that Oprah will go (Just to be clear on that, since it's been a widely circulated rumor) " ilisomeka email ya msemaji wa Obama.

Lakini kifuta machozi ni kuwa, ugeni huo unatarajiwa kuchagizwa na uwepo wa Muimbaji mwenye asili ya Senegal, AKON pamoja na mkongwe wa muziki kutoka nchini Zimbabwe, Oliver Mutukudzi.

Taarifa za Oprah kwenda Kenya zagonga mwamba

Friday, 15 June 2018



Kampuni moja Marekani yajitolea kugawa ticket za show ya Beyonce na JAY-Z kwa wote ambao watakubali kupima HIV

Kampuni ya kujitolea inayotoa huduma za afya kupitia kituo cha Palmetto Community Care imekuja na kampeni ya kuhimiza watu kwenda kujua afya zao, imetangaza kuwa itakuwa inagawa ticket za show za #Beyonce na #JAY-Z kwa watu ambao watajitolea kwenda kupima 


Hii kampuni ina gari la huduma ambalo linazunguka sehemu mbalimbali kama vituo vya mabasi, club za usiku, kwenye matamasha na matukio mbalimbali kuwafata watu ambao wataamua kupima kwenye mji wa South Carolina, Marekani

Kampuni yajitolea kuwalipia mashabiki show ya Jay Z,Beyonce

Wednesday, 13 June 2018



Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un adaiwa kwenda nchini Singapore huku akiwa na choo cha kuhamishika katika gari lake na hotelini alipofikia.

Kwa mujibu wa mtandao wa Washington Post Kim Jong Un aliyefika na gari aina ya Mercedes Benz S600 likiwa na choo cha kuhamishika.

Watafiti mbalimbali wamedai kuwa uamuzi wa Rais Kim kutembea na choo chake ni kuepuka na choo chake kuchukuliwa na kuchunguzwa na maadui wake.

Rais Kim Jong Un alivyosafiri na choo chake