Serikali
ya Kenya imeitumia barua serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ikitaka ufafanuzi kuhusu suala la vifaranga vilivyoteketezwa hivi
karibuni ambavyo vinadaiwa kuingizwa nchini kutokea Kenya.
Taarifa
ya serikali kupitia wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, imetibitisha kupokea barua hiyo huku serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ikiahidi kuijibu na kuitolea ufafanuzi kama
ilivyofanya mwanzo.
“Vile
vile serikali imepokea barua kutoka Serikali ya Kenya kuhusu masuala
haya, na Serikali itaijibu barua hiyo kutoa ufafanuzi,”. imeeleza sehemu
ya taarifa ya wizara juu ya ufafauzi kuhusu suala la vifaranga pamoja na
mifugo iliyoingizwa nchini bila kufuata sheria.
Aidha
serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuhakikisha inafuata sheria
zote bila kuathiri uhusiano wake na nchi zingine, huku ikizitaka nchi
zote duniani, ikiwemo Kenya, kufuata miongozo ya WTO na Shirika la Afya
ya Wanyama Duniani (OIE) kwa kutoa vibali (export permit) kwa mtu yeyote
anayetaka kusafirisha mifugo nje ya nchi.
Kabla
ya kuteketezwa kwa Vifaranga hivyo serikali imesema Mkurugenzi wa
Huduma za Mifugo Tanzania alimpigia simu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo
wa Kenya kutaka kujua kama Mamlaka za Kenya zina habari kuhusu vifaranga
hivyo ili virudishwe lakini alisema hana taarifa kuhusu vifaranga hivyo
na kwamba Kenya haiko tayari kuruhusu vifaranga hivyo kurudishwa nchini
mwao.
0 comments:
Post a Comment