Wednesday 22 November 2017

Polisi walifunga jarida la Red Paper nchini Uganda


Polisi nchini Uganda wamelifunga gazeti maarufu la kubwa la udaku The Red Pepper, na kuwatia mbaroni baadhi ya wandishi wake.
Wakurugenzi wakuu watano wa gazeti hilo wanazuiliwa na polisi, kwa pamoja na wahariri kadhaa.
Hii inafuatia taarifa zilizochapishwa na gazeti hilo, inayodai kuwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni alikuwa akipanga njama za kupindua utawala wa Rwanda.
Madai hayo yamekanushwa na serikali ya Uganda.
Katika siku kadhaa za nyuma, Gazeti hilo la Red Pepper, limewahi kukumbwa na utata kadhaa.

0 comments:

Post a Comment