Staa wa soka wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano
Ronaldo usiku wa December 7 2017 amefanikiwa kutangazwa mshindi wa tuzo
ya Ballon d'Or na kuwashinda Lionel Messi wa FC Barcelona na Neymar wa
Paris Saint ya Germain ya Ufaransa. Tuzo hiyo imezidi kudhihirisha kuwa
Ronaldo ni mmoja kati ya wachezaji bora wa muda wote katika soka, hiyo
inatokana na kujizolea tuzo kubwa ikiwemo ile ya mchezaji bora wa FIFA
aliyoshinda mwezi Oktoba mwaka huu 2017. Ronaldo ameshinda tuzo ya tano
ya Ballon d'Or akiwa na Real Madrid lakini tuzo yake ya kwanza ya Ballon
d'Or inayoandaliwa na France Football Magazine alishinda mwaka 2008
akiwa amefunga jumla ya magoli 42, akitwaa Champions League na taji la
Ligi Kuu England EPL. Hata hivyo Ronaldo ameeleza nia yake ya kutaka
kushinda Ballon d'Or mara saba na kupata watoto saba ndio malengo yake
kama ambavyo anatumia namba saba uwanjani lakini pia ni nembo yake ya
biashara.
0 comments:
Post a Comment