Friday 15 December 2017

Zanzibar na Uganda Cranes nusu fainali leo CECAFA

 

Kuhusu mechi ya pili ya nusu fainali inayopigwa leo mjini Kisumu, kocha mkuu wa Zanzibar Hemed Suleiman amesema, kwa kutumia vipaji alivyonavyo kwenye kikosi chake watajitahidi kutafuta matokeo mazuri kwenye mechi dhidi ya Uganda, ili kuendeleza rekodi nzuri waliyopata kwenye mashindano ya msimu huu.

Lakini kwa upande wake kocha wa the Cranes, Moses Basena, yeye amekiri mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi za hatua ya makundi, na kwamba kupitia uzoefu walionao kwenye michuano hiyo watajitahidi kushinda mechi hiyo ili kuingia fainali.

0 comments:

Post a Comment