Mwandishi wa Habari za vikaragosi/Vikatuni nchini Tanzania, Masoud Kipanya amejitokeza hadharani baada ya taarifa za kushikiliwa na kusambaa mitandaoni jana Januari 01, 2018 taarifa kuwa Masoud Kipanya amekamatwa na watu wasiojulikana ambapo hata kampuni ya Clouds Media Groups ilishindwa kutolea maelezo ya kina ya taarifa hizo.
Kipanya amethibitisha taarifa hizo za kupatikana kwake kupitia kurasa zake za mitanda ya kijamii ameandika kuwa anamshukuru sana mtu aliyesambaza taarifa za kukamatwa kwani ndio zimemuokoa.
“Poleni kwa usumbufu na asanteni kwa kujali hali za wengine. Niko salama Alhamdulillah. Namshukuru pia aliyesambaza taarifa. ‘AMESAIDIA’.“ameandika Masoud Kipanya.
0 comments:
Post a Comment