Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu, amewasili salama nchini Ubelgiji alikokwenda kwa ajili ya matibabu.
Mhe. Lissu akiwa uwanja wa ndege wa Brussels, Ubelgiji.
Kwa mujibu wa afisa huyo wa serikali nchini Ubelgiji, Lissu alipokelewa uwanja wa ndege chini ya ulinzi mkali wa maofisa wa polisi na wale wa usalama.
Lissu aliingia nchini humo kwa ndege ya shirika la ndege la Uholanzi (KLM), ambayo ilimchukua kutokea Amstedam, Uholanzi.
Mhe. Lissu alianza safari yake ya matibabu ya tatu alitokea Nairobi, Kenya kwa ndege ya shirika la ndege la nchi hiyo KQ, saa mbili asubuhi jana Jumamosi Januari 6, 2017.
Taarifa kutoka kwa wahusika wa msafara huo zimeeleza kuwa ulinzi umeimarishwa kwenye hospitali aliyofikia kwa ajili ya matibabu ambayo bado haijatajwa jina.
Mhe. Lissu alishambuliwa kwa risasi na wasiojulikana mnamo Septemba 7, 2017 nyumbani kwake Area D, mkoani Dodoma.
0 comments:
Post a Comment