Friday 26 January 2018

Rais wa Zimbabwe akutana na kiongozi wa IMF


Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amekutana na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la fedha la kimataifa IMF Bibi Christine Lagarde katika Mkutano wa Baraza la uchumi duniani WEF unaofanyika huko Davos, Uswisi.
Shirika hilo limesema katika taarifa yake kwamba Bibi Lagarde amekaribisha ahadi ya Rais Mnangagwa ya kuimarisha uchumi wa Zimbabwe na kufanya juhudi kuiunganisha nchi hiyo na jumuiya ya kimataifa, na shirika hilo litaendelea kuiunga mkono Zimbabwe kukabiliana na changamoto zake za kiuchumi.
Rais Mnangagwa anahudhuria mkutano wa Davos, kuitangaza Zimbabwe na kuvutia wawekezaji kusaidia kufufua uchumi baada ya kutengwa na jumuiya ya kimataifa kwa miaka mingi.

0 comments:

Post a Comment