Bingwa wa riadha kwa upande wa
wanawake nchini Afrika Kusini Caster Semenya ametajwa kuwania tuzo ya
mwanamichezo bora kwa upande wa wanawake duniani kwa mwaka 2017, tuzo
zinazojulikana kama Laureus World Sports Woman of the Year Award
itakayotolewa mjini Monaco nchini Ufaransa Februari 27 mwaka huu.
Katika tuzo hiyo kwa mwaka huu Caster anashindana na nyota wengine
duniani wakiwemo, wachezaji wa tennis Serena Williams wa Marekani,
Garbine Muguruza wa Hispania, bingwa wa michezo ya kuteleza kwenye
barafu Mikaela Shriffin wa Marekani na Chipukizi nyota katika mchezo wa
kuogelea kutoka Marekani.
Akitoa pongezi za serikali, Rais wa chama cha riadha cha Afrika Kusini, Alech Skhosana, pamoja na mambo mengine, amesema taifa zima lina imani na Caster, vile vile linaamini atatwaa tuzo hiyo, huku akimshukuru kocha wa mwanamichezo huyo ambaye ni bingwa mara tatu wa mbio za mita 800 wanawake duniani.

0 comments:
Post a Comment