Thursday 1 February 2018

Marekani yamwongeza kiongozi wa Hamas kama gaidi



Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imemwongeza kiongozi wa kundi la Hamas la Palestina Bw. Ismail Haniyeh kwenye orodha yake ya magaidi wa kimataifa. Jana kundi la Hamas limelaani uamuzi huo wa Marekani na kuutaja kuwa ni "hatua ya kuchekesha". Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Hamas Bw. Hazem Qassem amesema hili ni jaribio lililoshindwa la kushinikiza kukomesha mapambano ya kisilaha ya wapalestina, na kwamba hatua hiyo haitavunja dhamira yao ya kuendeleza mapambano hadi ukaliaji wa Israel kwenye ardhi ya Palestina utakapokomeshwa.

0 comments:

Post a Comment