Thursday 8 March 2018

Facebook,Whatsapp zazimwa Sri Lanka



Serikali ya nchini Sri Lanka imezuia Mitandao ya Kijamii ikiwemo Facebook na WhatsApp kufuatia kuendelea kwa vurugu za kidini nchini humo, licha ya kutangazwa kwa hali ya hatari
Mitandao hiyo ya Kijamii imepangwa kuzuiwa kwa muda wa siku tatu

Hali hiyo ya hatari ilitangazwa jana Machi 06, baada ya vurugu kutokana na Wabudha kuvamia Misikiti na biashara zinazomilikiwa na Waislam

Serikali imezitaka Kampuni zinazosambaza huduma ya Internet kuzima Mitandao ya Kijamii baada ya kuonekana inatumiwa kutuma jumbe za kichochozi za kutaka kuwashambilia Waislam
Takribani asilimia 70 ya watu nchini humo ni Wabudha na asilimia 10 ni Waislam

Mvutano kati ya jamii hizo mbili umeongezeka zaidi mwaka uliopita, ambapo Wabudha wamekuwa wakiwalaumu Waislam kushawishi Wabudha kubadili dini na kuwa Waislam

0 comments:

Post a Comment