Sunday 10 June 2018

Samuel Jackson na ndoto za kuwa ndani ya Filamu ya Black Panther



Mwigizaji maarufu kutoka nchini Marekani, Samuel L. Jackson kupitia kipindi cha Ellen Show amefunguka namna alivyokataliwa kushiriki katika filamu ya Black Panther.

Samuel ambaye ni mmoja kati ya waigizaji wanaofanya vizuri amesema kuwa kuna siku aliwaomba angalau wampe nafasi aonekane haa kwenye kipande cha dakika mbili tu katika filamu nzima lakini ombi hilo liligonga mwamba.


Kutokana na filamu ya Black Panther kuonekana kufanya vizuri kwa kipindi kifupi tu imeanza mchakato wa kutoa sehemu ya pili na huenda Samuel akaonekana.

0 comments:

Post a Comment