Tuesday 5 June 2018

Trey Song akabiliwa na shtaka jipya la kumshambulia polisi mwaka 2016



Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani,
Trey Songz anakabiliwa na shtaka jipya baada ya askari mmoja kutoka mji wa Detroit kudai kupigwa ngumi na msanii huyo Desemba 2016!
Kwa mujibu wa mtandao wa @TMZ_Tv inaripoti kuwa Sgt. Robert Avery amesema kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa kama mlinzi katika matamasha makubwa na katika  matamasha ya Trey katika Joe Louis Arena tarehe 28 Desemba 2016 lakini tukio a upigwa na msanii huyo limekuwa likimsumbua sana na kuona kama amedhalilishw kwa kiasi kikubwa.

 
Tukio la kupigwa ngumi lilianza baada ya Trey Song kutaka kumshambulia mpig picha ndipo Sgt. Avery aliamua kuingilia kati na hapo akakutana na shambulio la ngumi dhidi yake,amesema kwamba mwimbaji huyo alimpiga ngumi ambayo imesababisha kuanguka chini na kugonga kichwa chake juu ya saruji.

0 comments:

Post a Comment