Sunday 5 August 2018

Clarence Seedorf Kocha mpya Cameroon



Cameroon imemtangaza Clarence Seedorf(42) kuwa Kocha mkuu wa timu ya soka ya Taifa hilo baada ya kutofikia makubaliano na Kocha waliyekuwa wanamuwinda kwa muda, Sven-Goran Eriksson

Mchezaji huyo wa zamani wa vilabu vya Real Madrid na AC Milan pamoja na timu ya Taifa ya Uholanzi atasaidiwa na mchezaji mwenzake wa zamani katika timu ya Taifa, Patrick Kluivert

Muda wa mkataba atakaosaini Seedorf na Cameroon ambao ni mabigwa mara tano wa michuano ya Mataifa ya Afrika utatangazwa baadae mwezi huu

Awali Seedorf amewahi kuvifundishwa vilabu vya AC Milan, Chinese Club Shenzhen na Deportivo La Coruna ambapo alidumu wa muda usiozidi miezi 6 katika kazi zote hizo

0 comments:

Post a Comment