Friday 10 November 2017

Apanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia baiskeli ndani ya siku tano



Juanito Oiarzabal na wenzake wawili wamekamilisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia saa 31 ndani ya siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru baada ya kufika huko huku akiendesha baiskeli
Safari ya wageni hawa, Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia kupanda Mlima mkubwa kulikoyote barani Afrika na wapili kwa urefu duniani kwa kutumia Baiskeli ilianzia kupitia lango la Kilema.

Juanito Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole kutokana na barafu katika Milima mbalimbali aliyopanda amesema changamoto aliyokutana nayo wakati wa kupanda mlima ni kuzoea hali ya hewa ya mlima ambayo imekuwa ikibadilika kila wakati.

0 comments:

Post a Comment