Msanii wa R&B, nchini Tanzania Ben Pol yupo nchini Ufaransa katika mji Paris kwaajili ya kuhudhuria halfa maalumu iliyoandaliwa na taasisi ya Maua.
“Jana niliwasili mjini Paris (France) kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalum iliyoandaliwa na taasisi ya MAÜA Association, itakayofanyika tarehe 18 Novemba 2017 mjini humu.
Hafla hiyo itaambatana na utambulisho rasmi wa BenPol kama balozi mpya wa MAÜA association.,” aliandika Ben Pol Instagram.
“Sherehe hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Wana-diaspora, viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,”
“Maüa association (MAÜA) ni taasisi iliyoundwa na kusajiliwa nchini Ufaransa kwa minajili ya kutoa usaidizi wa kiafya kwa watoto na vijana ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao. #feelingood #feelingloved#godbless ,” aliongeza muimbaji huyo.
0 comments:
Post a Comment