Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa kitabadilisha fikra
za wananchi pamoja na mazoea ya kwenda hospitali pale wanapokuwa
wanaumwa na badala yake watawajengea uwezo wa kwenda hospitali mara kwa
mara ili kujua Afya zao.
Hayo
yamesemwa na Katibu wa CHADEMA Dar es salam na Mjumbe Baraza kuu na
Mkutano Mkuu Taifa Henry Kilewo ambaye amesema pamoja na kuwajengea
uwezo wananchi watatoa na bima za afya kwa wananchi.
"Chadema
tutakapokuwa Tunaongoza Nchi 2020 tutabadili Fikra za Mazoea Kwa
Wananchi kusubiri Kuumwa ndiyo waende Hospital,Tutawajengea Uwezo wa
Kucheki Afya Zao Mara kwa Mara pamoja na kuwapatia Bima za Afya" Kilewo.
Mbali
na hayo Kilewo amefafanua kwamba ni muda muafaka kwa serikali kuwekeza
kwenye Sekta ya Afya mahali ambapo panadaiwa kuwa na changamoto huku
akikosoa namna Tanzania ilivyo nyuma kwenye sekta ya afya.
"Ni
aibu na dhihaka kwa Taifa kwa watu kujazana kwenda kupata matibabu
kwenye meli ya wachina, hii inaonyesha ni namna gani tulivyo nyuma
kwenye Sekta ya Afya...Viongozi wetu kama wanashabikia hili basi Taifa
lipo kwenye msiba mkubwa wa uongozi,Taifa linalia". Ameandika Kilewo
kwenye ukurasa wake wa Twitter
0 comments:
Post a Comment