Tuesday 21 November 2017

WIZKID ATANGAZA MTOTO WA TATU


WIZKID ATANGAZA MTOTO WA TATU


Huu ni mwezi wenye matukio mengi kwa pop star kutoka Nigeria, Wizkid. Wizkid atangaza ujio wa mtoto wake wa tatu kupitia tweet yake aliyoandika jina la mtoto "Zion Ayo Balogun"



Zion anakua mtoto wa tatu kwa wizkid wa kwanza ni Boluwatife aliyezaa na Sola Ogudu mwaka 2011 na mwaka 2016 alitangaza kupata mtoto wa pili aliyezaa na mwanamitindo kutoka marekani mwenye asili ya Guinea, Binta Diamond Diallo.


Na safari hii amezaa na manager wake aliyekua anafanya nae kazi kwa kumsaidia kutafuta connection mbalimbali na wasanii wa kimataifa,Jada Pollock.


Jada Pollock mrembo mchapakazi kutoka uingeleza kupitia brand yake consultancy business ameshafanya kazi na mastaa mbalimbali duniani akiwemo mchezaji wa zamani wa Chelsea mshambuliaji Didier Drogba na wasanii Kama Chris Brown na Pia Mia.


Wizkid alianza kufanya kazi na Jada mwaka 2014 na ndio ulikua mwanzo wa Wizkid kupasua mziki wake kimataifa zaidi. Jada alimuunganisha Drake na Wizkid na kufanya remix ya Ojuelegba.


Jada mwenye umri wa miaka 34 alianza kuwa mwanamitindo lakini baada ya kumaliza degree yake ya biashara kutoka chuo cha Westminster alianza kujitegemea mwenyewe kwa kuanza biashara mbalimbali.


Jada alipata ujauzito toka Valentine Day mwaka huu na alijifungua wiki mbili zilizopita na kufanya siri mpaka Jana alipotangaza kuwa na mtoto.




0 comments:

Post a Comment