Kiongozi wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amtakia kila heri aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana chadema Bavicha, Patrobas Katambi ambaye ametangaza
kujiunga na CCM kwa kuwa ni haki ya Kikatiba.
Akizungumza
jana Jumanne baada ya Katambi kuhamia CCM, Dk Mashinji alisema; “sisi
kama chama msimamo wetu tuliuweka tangu madiwani walivyoanza kuondoka,
tukaweka msimamo wazi kwamba, suala la mtu kuondoka kwenye chama au
kubaki ni suala la Katiba ya nchi ambayo inampa mtu uhuru wa kuhama na
kwenda kwenye chama anachotakana.”
Alisema kuwa haoni sababu ya kumzuia mtu kuondoka kwa kuwa mtu anapoamua kwenda sehemu yoyote anakuwa na matarajio.
Pia,
Dk Mashinji alisema anamtakia heri (Katambi) na kuwataka CCM kumtumia
katika sehemu ambavyo wanaona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania
wote.
“Hatuna
mgogoro wowote na kimsingi mimi nimtakie tu heri (Katambi) na wakipenda
(CCM) wamtumie kwenye eneo watakaloona anafaa kutumika kwa faida ya
Watanzania wote,” alisema
Hata Hivyo, Dk Mashinji alisema kuwa walikuwa wanamuandaa Katambi asaidie chama hicho kwenye kitengo cha sheria.
“Alikuwa
anamalizia masomo yake ili awe wakili na tulikuwa tumeshaanza kumuandaa
ili atusaidie kwenye kitengo cha sheria ndani ya chama,”
Katambi
alitangaza jana kujiunga na CCM mbele ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya
CCM (NEC) unaofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment