Wednesday 22 November 2017

OFFSIDE TRICK WAFUKUZWA JUKWAANI

 Kundi la wasanii wa muziki wa Tanzania kutoka visiwani Zanzibar, Off Side Trick, walishushwa jukwaani na kusababisha kufungwa kwa tamasha la utamaduni la Lamu huko Mombasa baada ya kucheza mtindo usiofaa wenye kukiuka maadili.

Mkurugenzi Msaidizi wa Nyumba ya Maonyesho wa Kenya, Bwana Athman Hussein, amesema kuna haja ya kuwahakiki wasanii kabla hawajapanda jukwaani kutokana na kitendo hicho cha kudhalilisha mji.

0 comments:

Post a Comment