Tuesday 14 November 2017

Kocha Uingereza amuhofia Neymar

Kocha wa Uingereza, Gareth Southgate amewaonya wachezaji wake kuwa macho na Neymar katika mchezo wao hapo kesho dhidi ya Brazili katika Uwanja wa Wembley.






Mchezaji wa timu ya Brazili, Neymar

Southgate anaamini kuwa Neymar ni mchezaji pekee katika ulimwengu huu mwenyethamani ya paundi milioni 200.

Nahodha huyo wa Brazili ameweka rekodi hiyo ya dunia wa paundi milio 200 baada ya kusajiliwa na klabu ya Paris Saint-Germain  akitokea timu ya Barcelona ya nchini Hispania.

Uingereza ilitoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kirafiki siku ya Ijumaa ilipocheza na Ujerumani kocha Southgate anaamini kucheza na timu kama hizo itaifanya kuwa na kiwango bora zaidi katika dunia.

0 comments:

Post a Comment