Kikao cha
kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na washtakiwa wa uhalifu wa kivita
mjini The Hague, Uholanzi kimesitishwa ghafla baada ya mmoja wa
washtakiwa kusema amekunywa sumu baada ya kusikiliza hukumu.
Slobodan
Praljak, 72, alikuwa mmoja wa viongozi sita wa zamani wa kisiasa na wa
kijeshi wa Bosnia wa asili ya Croatia ambao walikuwa wamefika
mahakamani.Amefariki akitibiwa hospitalini na Umoja wa Mataifa umesema sasa mahakama hiyo ni "eneo la uhalifu".
Alikuwa amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 mnamo 2013 kwa makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa katika mji wa Mostar.
Baada ya kusikiliza hukumu kwamba majaji walikuwa wamedumisha kifungo hicho, alimwambia jaji, "Nimekunywa sumu".
Sita hao walikuwa wanasikiliza uamuzi wa mwisho wa rufaa uliokuwa unatolewa na mahakama maalum ya kimataifa ya UN iliyokuwa inashughulikiwa makosa yaliyotekelezwa Yugoslavia (ICTY).
Ingawa walikuwa washirika dhidi ya Waserbia wa Bosnia wakati wa vita hivyo vya 1992-95, Wacroatia wa Bosnia na Waislamu walipigana wenyewe kwa wenyewe kwa miezi 11.
Mji wa Mostar ulishuhudia mapigano makali zaidi.
Praljak alisimama na akainua mkono wake hadi kwenye kinywa chake, kisha anainamisha kichwa chake nyuma na kuonekana kunywa kitu kutoka kwenye gilasi ndogo.
Jaji mwandamizi Carmel Agius mara moja alisitisha shughuli na gari la kuwabeba wagonjwa likaitwa.
"Sawa," jaji alisema. "Tunaahirisha ki...Tunaahirisha...Tafadhari, pazia. Usiondoe gilasi ambayo ameitumia alipokunywa kitu."
Kabla ya pazia kurejeshwa, ukumbi wa mahakama umeonekana kujawa na mkanganyiko, anasema
Gari la kuwabeba wagonjwa lilionekana baadaye likifika nje ya ukumbi wa mahakama huku helikopta ikipaa juu angani.
0 comments:
Post a Comment