Sunday 12 November 2017

NECTA Wawapa onyo shule binafsi


Katibu Mkuu wa Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA),  Dr. Charles Msonde ametoa onyo kwa wamiliki wa shule binafsi nchini kutofanya udanganyifu katika mitihani ya kidato cha pili inayotarajiwa kuanza Kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari Dr. Msonde amesema kuwa wamiliki wanatakiwa kuheshimu vituo vya mitihani kwani kukiuka miiko uliowekwa na Baraza itapelekea kufungiwa.

"Upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili nchini utafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 24 Novemba, hivyo basi nawakumbusha wamiliki wa shule binafsi watambue kuwa shule zao ni vituo vya mitihani, nidhamu ya hali ya juu inahitajika katika kipindi chote cha zoezi hilo", amesema Dr. Msonde
Aidha ameainisha kuwa jumla ya wanafunzi laki tano ishirini na moja elfu mia nane hamsini na tano wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha pili 2017.

0 comments:

Post a Comment