Tuesday 21 November 2017

Nyashinski adai kulipwa 20m kwenye interview

 

Tuhuma hizo zimeibuka kupitia gazeti maarufu nchini Kenya la Pulse baada ya msanii huyo kudaiwa kutaka kulipwa kiasi cha shilingi milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na milioni 20 za Kitanzania katika kila interview atakayoalikwa.

“Alisema anataka tumlipe ndio aje kwenye show. Asipochunga ata-fade haraka. Nasikia amekuwa akiifanya hata studio fulani hivyo. Kwani yeye ni nani?,” limeandika gazeti hilo wakati wakimnukuu mmoja ya waaandishi ambao walikataliwa na Nyashinski kufanya mahojiano.

Nyashinski amedaiwa kuwa alikataa kufanya mahojiano hayo na kipindi kikubwa nchini humo cha runinga ambacho kinaruka kila siku za Ijumaa usiku.

0 comments:

Post a Comment