Jeshi
la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa Jeshi la Magereza,
Faustine Masanja, kwa tuhuma za kumwua kwa kumpiga risasi askari
mwenzake, wakiwa kazini.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo, alisema tukio hilo
lilitokea jana asubuhi katika eneo la Magereza, Kisongo nje kidogo ya
jiji la Arusha.
Mkumbo alimtaja marehemu kuwa ni Ombeni Mwakiyani.
Alisema
siku ya tukio wakiwa kazini, Faustine alidaiwa kumjeruhi askari
mwenzake ambaye alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika
Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
“Tukio
limetokea asubuhi…Faustine alimjeruhi mwenzake wakiwa kazini na baada
ya kumjeruhi alipelekwa hospitalini kupata tiba ila alifariki dunia.
“Tunachunguza kubaini nini hasa chanzo cha kumjeruhi mwenzake na kumsababishia kifo,” alisema Kamanda.
Mmoja
wa askari magereza aliyeshuhudia tukio hilo, alidai Masanja na
Mwakiyani wameoa katika familia moja na inadaiwa kulikuwa na ugomvi wa
familia kati yao.
Chanzo hicho kilidai asubuhi wakiwa kazini, Faustine alimpiga mwenzake risasi ya nyuma ya kichwa ambayo ilitokea usoni.
“Wameoa
familia moja na wote wanakaa kambini na Faustine aligombana na mke wake
ambaye ameondoka nyumbani hivyo akawa anamtuhumu marehemu kupitia mke
wake kuwa walimjaza mkewe maneno na kusababisha aondoke nyumbani.
“Baada
ya kumpiga mwenzake risasi alitupa silaha yake chini na kusema akamatwe
wala hakimbii kwa sababu anajua ameua. Ila ugomvi wenyewe hatujajua
ulikuwa ni nini hasa,” kilisema chanzo
0 comments:
Post a Comment