Friday 15 December 2017

Waziri mkuu Uingereza ahimiza makubaliano umoja wa Ulaya kufanyika Brexit

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May anaelekea mjini Brussels hii leo ambapo atawahimiza viongozi wa Umoja wa Ulaya kuidhinisha makubaliano ya kusogeza mbele mazungumzo ya Brexit katika awamu ya pili.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May anaelekea mjini Brussels hii leo ambapo atawahimiza viongozi wa Umoja wa Ulaya kuidhinisha makubaliano ya kusogeza mbele mazungumzo ya Brexit katika awamu ya pili, akieleza kuwa ni mpango wa haki unaotoa msingi mzuri wa majadiliano ya mahusiano ya baadae.
Mwanzoni mwa chakula cha jioni mjini Brussels, saa 24 baada ya matokeo ya kushangaza ya bunge nyumbani, waziri mkuu May atarudia hoja yake ya kufungua mazungumzo ya kufumua zaidi ya miaka 40 ya muungano ili kuruhusu majadiliano ya biashara ya baadae, ambayo anaona kama ni muhimu katika kutoa uhakika wa biashara.
Viongozi wengine 27 wa Umoja huo wote lakini wana uhakika wa kuthibitisha mpango wa kusonga mbele katika awamu ya pili siku ya kesho Ijumaa, baada ya May kuondoka mjini Brussels, akianzisha hatua nyingine ya mazungumzo yanayoweza kuzuiwa na mgawanyiko nyumbani na tofauti ndani ya Umoja wa Ulaya.
England Parlament stimmt über Brexit ab (picture alliance/dpa/AP Photo) Bunge la Uingereza katika mjadala mkali wa Brexit
Kura ya bunge 
Katika pigo lingine kwa May, ambaye tayari amedhoofika baada ya kupoteza wingi wa viti katika chama cha Conservative kwenye uchaguzi wa Juni, bunge hapo jana limepiga kura ya marekebisho ambayo yanahitaji kura ya maana ya bunge hapo baadae juu ya mpango wowote wa mwisho wa Brexit. Hadi dakika ya mwisho ya mjadala mgumu, timu ya May ilijaribu kuwashawishi wabunge katika chama chake ili kuzuia hoja hiyo, ambayo serikali inaona kwamba itadhoofisha mkono wake katika majadiliano ya Brexit. Lakini wabunge wa kutosha wa Conservative waliasi na kushinda kwa kura 309 kuunga mkono mabadiliko ili kulipa bunge mamlaka ya kuamua juu ya Brexit na wabunge 305 waliyapinga mabadiliko hayo.
Baada ya kura hiyo, kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn amesema kwamba, "Hatimaye bunge limefany akazi yake. Waziri mkuu alijaribu kunyakua madaraka kwa nguvu, akijaribu kushinikiza muswada wa Umoja wa Ulaya bila ya kuzingatia bunge na kuchukua madaraka ya bunge, bunge limekataa na kushinda kura ambayo inasema lazima kuwepo na uamuzi sahihi wa bunge la Uingereza juu yamasharti na kitakachotokea juu ya majadiliano ya Brexit."
Mafanikio ya May 
Baada ya siku kadhaa za diplomasia, May aliweza kuokoa mpango wa mwisho Ijumaa iliyopita, na kutuliza wasiwasi wa mshirika wake Ireland ya Kaskazini juu ya kulinda uhuru wa mpaka na mwanachama wa Umoja wa Ulaya Ireland bila ya kutenga jimbo hilo kutoka Uingereza.

0 comments:

Post a Comment