Dkt.
Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu wake baada ya kutangaza dau kubwa la
kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda
kusihi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo.
Akizungumza
kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika
amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo
hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani
zitahamishiwa New York Marekani.
“Sasa
hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu halafu mimi nisepe, nikiwa
hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa
Bara la Afrika, sasa ni world wide, ofisi itakuwa New York,
nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR.
“Hata
mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza
nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania,
nimeteuliwa kwa veto power, hizi ziko tano kwenye umoja wa mataifa, jina
langu lilikuwa projected na Urusi na mwenyewe Rais Vladimir Putin”,
amesema Dkt. Shika.
Dkt.
Shika ameendelea kwa kusema kwamba kura ambazo alipata zilitosha kwa
yeye kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa, kwani nchi tatu zilikubali jina
lake kupitishwa ikiwemo na Marekani.
0 comments:
Post a Comment