Kijana huyo ambaye ni mgonjwa wa akili alifanyiwa upasuaji huo katika hospitali teule ya Missenye, Mugana na kukutwa pia na viberiti vya gesi, mfuko, vitambaa na ganda la limao
Dkt. Eliud Nyonyi aliyeshiriki kumfanyia upasuaji mgonjwa huyo, Eliud Novart(25) amesema baada ya vitu hivyo kutolewa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri
Mganga Mkuu wa Missenye, Dkt. Hamis Abdallah alisema mgonjwa alifikishwa katika Hospitali ya Mugana baada ya kupatiwa rufaa na Hospitali ya Nyakahanga, wilayani Karagwe
0 comments:
Post a Comment