Sunday 24 December 2017

Emmanuel Eboue kapokonywa Mali zote na mkewe.


Baada ya kusakata kabumbu la ligi kuu ya uingeleza kwa miaka Saba na kutengeneza mamilioni ya pounds, kumiliki majumba na magari ya kifahari kupitia kipaji chake, sasa hivi mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ivory Coast hana kitu mfukoni.

Eboue anaishi maisha ya kujificha, analala chini kwenye nyumba ya rafiki yake, hana usafiri na nguo anajifulia mwenyewe na mkono kwa kuwa hana hata hela ya kumlipa dobi.
Eboue ameshindwa kesi mahakamani ya kuachana na mkewe na kuchukuliwa mali zote na mkewe kwa sababu mali zote aliandikisha kwa jina la mke wake.

Eboue anajilaumu sana kwenye maisha yake kwa kitendo cha kumuamini mkewe na kumpa umiliki wa mali zake zote.
Eboue amekuwa ni mtu mwenye huzuni muda wote na anatamani hata kujiua akikumbuka alipotoka kwenye maisha duni na kujilaumu kwanini alichofanya.

Eboue anawashauri vijana wa Africa wajifunze kupitia makosa yake aliyofanya kwa kutenda jambo bila ya kufikiria.
Eboue alikuwa anaingiza kiasi cha Euro million 8 kwa mwaka, katika hizo hela Euro million 7 alikuwa anamkabidhi mkewe kwa ajiri ya familia na kila achokuwa anaambiwa na mkewe alifanya.
Prepared by @racathedon #eboue #life #arsenal #newschemba

0 comments:

Post a Comment