Saturday, 23 December 2017

Gabo Zigamba atoa sababu inayofanya Bongo movie kuanguka


Msanii Gabo Zigamba anayetamba katik tasnia ya Movie nchini ametema cheche juu ya wasanii wa tasnia hiyo kuanguka katika kazi.
Gabo alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz ndani ya televisheni ya Eatv na kusema kuwa tasnia hiyo inapoteza nguvu kutokana na wasanii wake wengi kujikita kufanya kazi zingine zisizohusiana na sanaa.
"Nikizungumza kwa mapana sana inaweza ikawa inawagusa baadhi ya watu ila wasisikitike bali wachukue namna ya kujifunza, unapoacha kazi yako ukafanya kazi ya mwenzako ina maana unaharibu kazi yako. Kazi ambazo zilikuwa zinafanywa na wengi katika wao ambao walikuwa wanafanya kazi zisizokuwa za kwao zinawachanganya watu, unajua hata ukiwa si mwanachuo ukaenda kuzindua majengo ya chuo unaweza ukawachanganya wakashindwa kutambua wewe taaluma yako nini" alisema Gabo Zingamba
Aidha Gabo Zigamba amewashauri wasanii hao njia nzuri itakayosaidia tasnia ya filamu kusonga mbele na wao wenyewe kuwa na heshima katika kazi zao ni pamoja na kufanya kazi yao na kuachana na kazi za watu wengine.
"Itumike hekima na watu waridhike na kubaki katika kazi yetu ya sanaa tusiambatane sana na kazi ambazo hazituhusu basi kuna uwezekano wasanii wa filamu wakawa wamefanikiwa lakini hata wapenda taaluma yetu wakawa wamefanikiwa" alisisitiza Gabo

0 comments:

Post a Comment