Timu ya kikapu ya Monaco ya Ufaransa imeendelea kujiimarisha katika uongozi wake
kwenye msimamo wa kundi A la mashindano ya ligi ya klabu bingwa barani
Ulaya baada ya kuifunga timu ya Juventus ya Italia kwa alama 92-85.
Monaco walifanikiwa kuongoza katika robo tatu za mchezo huo,
ambapo kupitia nyota wake Aaron Craft, Paul Lacombe na Abdel Kader Sylla
waliopata kwa pamoja alama 53, ilifanikiwa kuwavunja nguvu Juventus
ambao katika robo ya pili walirejea na makali na kuongoza kwa alama
24-20.
Juventus iko katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi hilo na inatarajiwa kucheza mechi nyingine dhidi ya Pinar Karsiyaka ya Uturuki inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo huo.
Juventus iko katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi hilo na inatarajiwa kucheza mechi nyingine dhidi ya Pinar Karsiyaka ya Uturuki inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo huo.
0 comments:
Post a Comment