Maseneta wa Marekani wanajadili mswada ambao unaweza kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa Kodi ambao umekuwepo kwa zaidi ya miongo mitatu nchini humo.
Wabunge wa bunge la wawakilishi awali walipiga kura upande wa mabadiliko makubwa ambayo ikiwa yatapitishwa itakuwa ni mafanikio ya kwanza makubwa ya Rais Trump katika utawala wake.Kura za Seneti zinategemewa kupigwa saa chache zijazo.
Kwa upande wa wabunge wa Democratic wanasema maamuzi hayo yanawanufaisha makampuni makubwa na matajiri.
Mswada huu ukoje?
Unatafsiriwa na Rais Trump kama zawadi ya sikukuu za Christmass na mwaka mpya kwa wananchi wote, huku mbunge wa Democratic Barbara Lee akisema ni sawa na kuzipiga kofi kali la usoni familia za kipato cha chini na kati.
Inatarajiwa kukata kodi kwa makampuni kutoka asilimia 35 mpaka 21.
Inapunguza kodi kwa mashirika makubwa sambamba na kima cha kati kwa makampuni mengine.
Inatarajiwa pia kupunguza kodi kwa watu binafsi.

0 comments:
Post a Comment