Wednesday 13 December 2017

Mbondia wanne Kenya watunukiwa Tuzo ya Heshima na Rais Kenyatta



Katika kuadhimisha sikukuu ya jamhuri nchini Kenya, jana Rais uhuru Kenyatta amewatunuku nishani za heshima mabondia wanne kutokana na umahiri wao pamoja na kuiletea sifa nchi yao kimataifa.
Mabondia waliopata tuzo hiyo inayojulikana kama Head of State Recommendation ni Fatuma Zarika, Rayton Okwiri, Maurice Okolla na James Onyango.
Wote hao tayari wameiwakilisha Kenya katika mapambano mengi ya kimataifa na kila mmoja akiwa tayari amegusa mkanda wa ubingwa wa WBO katika ngazi za Afrika Mashariki na Kati, Afrika na Duniani.

0 comments:

Post a Comment