Friday 1 December 2017

Merkel kukutana na hasimu wake ySchulz kwa mazungumzo


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefanya mazungumzo ya kwanza jana na mwenyekiti wa chama cha Social Democratic SPD, Martin Schulz, kuangalia uwezekano wa kuunda serikali ya mseto.
Bundestagswahl | Elefantenrunde Schulz und Merkel (imago/photothek/T. Imo)
Mkutano huo uliofanyika chini ya mualiko wa rais wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, umefanyika huku dhumuni kuu ni mstakabali juu ya siasa nchini humo pande hizo mbili ziko tayari kuanza mazungumzo ya serikali mpya. Baada ya uchaguzi wa mwezi Septemba kumuacha Merkel bila wingi wa wajumbe bungeni, chama cha SPD kilitangaza kwa ukaidi kwamba hakitaendelea kushirikiana na kansela huyo, baada ya kufanya vibaya sana na kupata matokeo ya kuabisha katika uchaguzi huo.
Lakini baada ya juhudi za Merkel kuunda serikali ya mseto na chama cha walinda mazingira cha Kijani na chama cha kiliberali kinachowapendelea wafanyabishara, FDP, kusambaratika, chama cha SPD kilikabiliwa na shinikizo la kubadili msimamo wake ili kuepusha uchaguzi wa mapema.
Jarida linalochapishwa kila wiki hapa Ujerumani, Der Spiegel, limedokeza kwamba mkutano wa leo utakaohudhuriwa pia na Horst Seehofer, mwenyekiti wa chama cha Bavaria cha Christian Social Union, CSU, ni wa umuhimu mkubwa kwa mwanasiasa siasa huyo mkongwe. Kwa kansela Merkel "ni vita vya kupigania mustakabali wake kisiasa ambavyo vinaanza" limesema jarida la Spiegel na kuongeza kuwa Merkel analazimika kufanya kila kitu kuunda muungano huu, ambao pekee utahakikisha mamlaka thabiti.
Akizungumzia mkutano huo Schulz amesema kujenga mustakabali mwema kwa Ujerumani ni jukumu la serikali ijayo. Hiyo haina maana kuongoza nchi bila mpango wa muda mrefu. Ina maana kufanya mageuzi muhimu ambayo itabidi yapiganiwe na kujadiliwa kwa kina.

0 comments:

Post a Comment