Monday 11 December 2017

Mourinho alalamika baada ya timu yake kufungwa na Man City

 Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amemlaumu mwamuzi wa mechi ya timu yake dhidi ya Manchester City, Michael Oliver, kuwa yeye ndiye aliyapelekea timu yake kufungwa.

Mourinho amesema mwamuzi huyo aliinyima timu yake penati ya wazi ambayo ingesawazisha matokeo ya 2-1 yaliyoimaliza timu yake.
Licha ya shutuma hizo kwa mwamuzi, Mourinho ametamka kuwa Man City wamepata kwa kuwa jana ilikuwa ni siku yao ya bahati.
Kwa upande wake, kocha wa City, Pep Guardiola, amesema anaridhishwa na kiwango cha timu yake, na ndiyo maana wanapata ushindi.
City sasa, wanafikisha alama 46 killeleni ikiwa ni 11 zaidi ya United walio katika nafasi ya pili.

0 comments:

Post a Comment