Monday 11 December 2017

Jeshi la wananchi Tanzania lasema kamwe haliwezi kuacha kuunga mkono juhudi za kulinda amani Kongo

 

Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuuawa kwa askari wake 14 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hakutaifanya Tanzania iache kuunga mkono shughuli za ulinzi  na amani nchini humo.

Mnadhimu mkuu wa jeshi hilo luteni jenerali James Mwakibolwa amesema hayo baada ya kuuawa kwa askari hao kumeipa motisha Tanzania kuunga mkono juhudi za kulinda amani za Umoja wa mataifa. Amelitaja tukio hilo kama mauaji mabaya kabisa dhidi ya jeshi la Tanzania tangu mwaka 2011.
Amesema askari wa Tanzania waliuawa kwenye mapambano yaliyodumu kwa muda wa saa 13.
Askari waliouawa ni sehemu ya askari 3,000 wa tume ya kulinda amani ya umoja wa mataifa MONUSCO yenye askari kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
"Kuuwawa kwa wanajeshi wetu kamwe hakuwezi kuondoa motisha kwa wanajeshi wetu waliopo nchini Kongo,"alisema.

0 comments:

Post a Comment