Mwanasheria
Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo amekamatwa na
serikali baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali .
Mwanasheria
huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo
pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake
bila kufuata sheria ya mazingira .
Akiwa
katika katika ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Geita,Mhe.Kangi
Lugola ameagiza kukamatwa kwa mwanasheria huyo baada ya kudaiwa kukutwa
na nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika kutoka taasisi ya
wakala wa utafiti wa jiolojia Tanzania(GST).
Hata
hivyo katika hali isiyo ya kawaida na bila kutarajiwa.Mwanasheria huyo
aliyekuwa akiukingia kifua mgodi huo ili usikumbane na rungu la fidia ya
uharibifu wa kimazingira kama sheria inavyotamka, alijikuta akimweleza
Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai haijaeleza iwapo mgodi
huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi huo usibebeshwe
mzigo huo.
Kutokana
na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe ripoti hiyo ili
ajiridhishe,lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka
kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake kuipata Serikalini, lakini yeye
hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo lililomkasirisha Naibu Waziri wa
Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.
Diwani
wa kata ya mtakuja Constatine Morandi ameelezea kuwa wananchi wamekuwa
wakisumbuliwa muda mrefu na mgodi bila ya kupatiwa fidia na kwamba
kutokana na wao kuwa ndani ya bikoni kumesababisha kutokupatiwa huduma
mbali mbali za kijamii hivyo ni vyema kwa serikali wakaweka nguvu
kuwasaidia wananchi hao.
Bw
Abdallah Omary-Mkazi Nyamalembo alimweleza Naibu waziri kwamba wamekuwa
wakiishi maisha ya mashaka kutokana na hali ilivyo ya maeneo hayo ya
mgodini na kwamba mgodi ulikwisha wai kuwapatia fidia ya shilingi elfu
ishirini jambo ambalo limeonekana kuwa ni udhalilishaji kwani pesa hiyo
ni ndogo.
Kwa
upande wake Makamu wa Rais wa mgodi huo Saimon Shayo,alisema kuwa eneo
ambalo wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu suala la fidia hadi sasa
kuna nyumba mbili na kwamba fidia ya kwanza walilipa kiasi cha sh,Bilion
Moja na waliipatia serikali iweze kuwafidia wananchi
0 comments:
Post a Comment