Saturday 9 December 2017

Rais Magufuli awasamehe Babu seya na Papi kocha,huku wafungwa 8,157 wakiwa huru



Rais Dkt. John Magufuli ametoa msahama kwa famiia ya Nguza Viking  a.k.a Babu seya  na mwanaye Papii Kocha waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.
Pia Rais  Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 8,157 huku wafungwa 1828 watatolewa leo.
Akizungumza leo katika maadhimisho ya Miaka ya 56 ya Uhuru, Rais Magufuli huku akisema kuwa watu 6,329 watapunguziwa muda wa kukaa jela.
“Ninatoa msamaha kwa wafungwa 8,157 na wafungwa 1,828 watatoka leo na 6,329 watapunguziwa muda wa kukaa jela,” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli alieleza kuwa amesamehe watu 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.


Rais Magufuli amesema hayo leo mjini Dodoma wakati wa sherehe za miaka 56 ya Uhuru. Pia Rais Magufuli ametoa msamaha kwa watu 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.
Nguza Viking na Papii Kocha walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya msingi.

0 comments:

Post a Comment