Saturday 9 December 2017

Wataalamu waishauri Uganda kutafuta ufumbuzi wa ndani kuhusu matatizo ya kiuchumi



Serikali ya Uganda imehimizwa kutafuta ufumbuzi wa ndani kuhusu matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo ,badili ya kutegemea ufumbuzi wa kigeni.
Katika hotuba yake katika kongamano la uchumi la NTV jijini Kampala jana,mwanauchumi na Mkuu wa Kitovu cha uwekezaji na biashara Afrika Mashariki cha USAID Bw Juan Estrada-Valle alisema Uganda inafaa kupiga jeki uchumi wake.
Alisema Uganda inahitaji kujitolea kwa malengo yake.Aliongeza kuwa ni muhimu kwa kila mtu kijijini kuelewa ni njia ipi nchi inachukua,na pia kufahamu jukumu lao katika maendeleo ya uchumi.
Aidha Estrada-Ville alisema waganda wanafaa kuanzisha mageuzi ya kiuchumi.

0 comments:

Post a Comment