Chama tawala nchini Afrika kusini, ANC kinafanya uchaguzi mwishoni mwa juma, unaoonekana kuwa mgumu, kumchagua mrithi wa kiongozi wake Jacob Zuma, ambapo mshindi pia atakuwa na nafasi ya kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Chama cha ANC kitamtangaza mrithi wa rais wa sasa Zuma kuwa kiongozi wa chama Jumapili (17.12.2017), kikikamilisha mpambano mkali wa kuwania uongozi ambao unatishia kukigawa chama hicho ambacho kilianza kama vuguvugu la ukombozi miaka 105 iliyopita, ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1994.Makamu wa rais Cyril Ramaphosa , mwenye umri wa miaka 65, ambaye kwa kiasi kikubwa anapendelewa na masoko ya fedha, na Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenye umri wa miaka 68, waziri wa zamani na mwenyekiti wa halmashauri ya Umoja wa Afrika wametamalaki katika mpambano huo.
Makamu wa rais Cyril Ramaphosa
Sarafu
ya Afrika kusini ya rand imekuwa imara kwa asilimia mbili
baada ya mahakama kutoa hukumu kwamba maafisa waandamizi katika
majimbo mawili walioonekana kumuunga mkono Dlamini-Zuma
walichaguliwa kinyume na sheria na hawataruhusiwa kuhudhuria
mkutano huo."Ishara za mapema za ushindi kwa Cyril Ramaphosa, ambaye anapendelewa na wawekezaji zaidi, ametoa usaidizi kwa sarafu ya rand," John Ashbourne , mtaalamu wa uchumi wa Afrika katika taasisi ya Capital Economics amesema.
"Lakini wakati Ramaphosa anaungwa mkono kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wanachama wa chama hicho, matokeo yataamuliwa na watu wa ndani kisiasa, ambao huenda wakaamua kumuunga mkono mpinzani wake mfuasi wa siasa wa mrengo wa kushoto, Nkosazana Dlamini-Zuma.
Ramaphosa alishinda kwa wingi wa kura za kuteuliwa kuwa kiongozi wa chama, lakini wajumbe katika mkutano huo ulioanza JumamosiDisemba (16-12 hadi 20.12.2017) mjini Johannesburg hawafungwi na kura alizopigiwa na tawi la chama cha ANC lililomteua kuwa mgombea wao, ikiwa na maana kwamba bado haiko wazi iwapo anaweza kushinda nafasi hiyo.
Ramaphosa ameongeza hivi karibuni ukosoaji wa serikali ya Zuma iliyogubikwa na kashfa, wakati Dlamini-Zuma amesema umuhimu wake anauweka katika kuboresha uwezo wa Waafrika waliowengi.
Waungaji mkono Ramaphosa
Kwa waungaji wake mkono, mafanikio ya Ramaphosa kibiashara yanamfanya kuwa katika nafasi nzuri ya jukumu la kubadilisha hali ya uchumi wa nchi hiyo inayokabiliwa na ukosefu wa nafasi za ajira kwa asilimia 28 ya watu pamoja na kupunguziwa viwango vya uwezo wa kukopa.
0 comments:
Post a Comment