Saturday, 16 December 2017

Prince Harry na Meghan Markle ndoa 19 Mei 2018

Mwanamfalme Harry na Meghan Markle watafunga ndoa mnamo Jumamosi 19 Mei, 2017, Kasri la Kensington limetangaza.

Wawili hao walithibitisha rasmi uchumba wao Novemba na wakasema harusi yao itafanyika katika kanisa ndogo la St George, Windsor Castle.
Tarehe ya harusi yao inaenda kinyume na utamaduni wa harusi za familia ya kifalme Uingereza ambazo hufanyika katikati ya wiki.
Harusi ya Malkia Elizabeth iliandaliwa Alhamisi nayo ya Mwanamfalme William ikafanyika Ijumaa.
Harusi hiyo itakuwa siku moja na fainali ya Kombe la FA, ambayo kwa kawaida Mwanamfalme William huhudhuria kama rais wa chama cha soka England, FA.
Wakati ambao mechi hiyo itachezwa bado haujatajwa, lakini kawaida huanza saa 17:30 GMT.
Familia ya kifalme nchini Uingereza itagharimia harusi hiyo, ikiwa ni pamoja na ibada yenyewe, muziki, maua na sherehe ya baada ya ibada.
Bi Markle, ambaye ni mprotestanti, atabatizwa na kupewa kipaimara kabla ya harusi hiyo kufanyika.
Mwigizaji huyo Mmarekani pia anakusudia kuchukua uraia wa Uingereza.
Afisa wa mawasiliano wa Mwanamfalme Harry Jason Knauf alisema mwezi jana kwamba Windsor ni "pahala maalum sana" kwa wawili hao, akisema walikaa huko kwa muda tangu walipokutana mara ya kwanza Julai 2016.
Mapema wiki hii Kensington Palace ilitangaza kwamba wawili hao watakaa pamoja na Malkia Elizabeth Sandringham wakati wa Krismasi.

Haki miliki ya picha PA

0 comments:

Post a Comment