Wednesday, 20 December 2017

Tume ya pamoja ya AU-EU-UN yadhamiria kupambana na Utumwa

 

Tume ya pamoja ya Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mambo ya uhamiaji, imeahidi kuimarisha utaratibu katika kupambana na biashara haramu ya binadamu na mtandao wa uhalifu.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika inasema, tume hiyo hivi karibuni imejadili njia ya kutatua suala la uhamiaji nchini Libya.
Kazi ya tume hiyo ni kushirikiana na serikali ya Libya inayotambulika kwa lengo kuu la kupambana na biashara haramu ya binadamu na mtandao wa uhalifu, na kuzisaidia nchi wanazotoka na wanazopita wahamiaji kutatua vyanzo vya uhamiaji vinavyotafuta fursa za maendeleo na utulivu.

0 comments:

Post a Comment