Bongo Fleva queen diva Vanessa Mdee amefunguka juu ya kuachia albamu yake mpya na lebo kubwa Duniani ya Universal Music Group.
Msanii huyo anayetamba na kibao cha 'Bounce' alichowashirikisha wasanii wawili nchini Maua sama na Tommy Flavor amesema hayo baada ya kutangaza kusaini mkataba na kampuni hiyo kubwa ya muziki duniani ambayo itakuwa inasimamia kazi zake katika Ulaya na Afrika.
Akizungumza na Social Buzz ya Clouds TV, muimbaji huyo amesema albamu hiyo itatoka mwezi wa sita mwakani chini ya kampuni ya Universal ambapo kwa mkataba wa aina yake ambao amesaini unamfanya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kupata dili nono kama hilo katika kampuni hiyo.

0 comments:
Post a Comment