Friday, 22 December 2017

Vyama vya siasa nchini Sudan Kusini vyasaini makubaliano ya kusimamisha mapigano

Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi nchini humo wamesaini makubaliano mapya ya kusimamisha mapigano yaliyodumu kwa miaka minne. 

 

 Makubaliano hayo yamesainiwa jana mjini Addis Ababa, Ethiopia, baada ya mazungumzo ya amani yaliyoongozwa na Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki IGAD yaliyoanza jumapili wiki hii.

Wakati huohuo, mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amepongeza kusainiwa kwa makubaliano hayo. Amesema hiyo ni hatua ya kwanza katika juhudi za kumaliza mapigano na vurugu zinazoendelea nchini Sudan Kusini tangu mwezi Disemba mwaka 2013. Hata hivyo amesisitiza kuwa jaribio halisi kuhusu udhati wa ahadi ya pande hizo husika ni katika utekelezaji wake kikamilifu, kumaliza vurugu na kudumisha sheria muhimu za kibinadamu za kimatifa.

0 comments:

Post a Comment