Thursday 4 January 2018

Alicia Keys aikacha kesi ya utapeli ya mumewe

Mnamo September 2017, mawakili wa Metro Gem Leasing walifungua mashtaka dhidi ya kampuni ya Swizz beats, 39, na Alicia ya AK Worldwide Productions wakidai mastaa wameshindwa kulipa ada ya magari walilowakodishia na wametapeli kampuni hio.

Msanii  wa muziki Marekani Alicia Keys ameomba kutolewa kwenye kesi ya madai ya dola milioni $16.5 anazotakiwa kulipa mume wake Swizz Beatz kwa kampuni ya magari ya kifahari nchini humo.
Alicia Keys na mume wake walipewa magari matano, ikiwemo Range Rover na Ferrari F12.
Alicia Keys anasema jina lake litolewe kwenye kesi hio sababu hakuhusika kwenye makubaliano, pia anajua magari yote yalirudishwa.
Mawakili wa Swizz wameshaomba kesi hii kufutwa sababu kampuni hio ya kukodi magari inataka kupata pesa kupitia umaarufu wa Swizz Beats.

0 comments:

Post a Comment