Thursday 4 January 2018

Ousmane Dembele kurejea dimbani baada ya kuwa majeruhi miezi minne

 

Mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi na Barcelona Ousmane Dembele huenda akarejea kucheza wiki hii baada ya kukaa nje ya uwanja wa karibu miezi minne.

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye miaka 20 alijiunga na Barca Agosti kwa £96.8m lakini akaumia akichezea klabu hiyo mechi yake ya tatu - dhidi ya Getafe mnamo 16 Septemba.
Dembele alifanyiwa upasuaji nchini Finland.
Sasa, huenda akarejea kucheza dhidi ya Celta Vigo katika Copa del Rey Alhamisi.

Viongozi wa ligi Barcelona kisha watakutana na Levante katika La Liga Jumapili.
Barca ambao wamo alama tisa mbele kileleni kwenye ligi wamepangiwa kukutana na Chelsea hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Februari na Machi.
Dembele - aliyejiunga nao kutoka Borussia Dortmund - ndiye mchezaji wa pili ghali zaidi duniani ba bei yake ya uhamisho inaweza kupanda hadi £135.5m.
Pesa walizolipa Barcelona mwanzoni zilikuwa karibu nusu ya £200m walizopokea kutoka Paris St-Germain kwa mshambuliaji Mbrazil Neymar.

0 comments:

Post a Comment