Klabu ya Barcelona imefuzu hatua
ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mfalme nchini Hispania (Copa Del
Rey) baada ya kuiondoa Espanyol kufuatia ushindi wa magoli mawili kwa
sifuri kwenye mechi ya marudiano ya robo fainali iliyofanyika jana.
Magoli ya Barcelona katika mechi hiyo yalifungwa na Lionel Messi moja na Luis Suarez moja.
Katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa Nou Camp, nyota Felipe Coutinho alicheza kwa mara ya kwanza katika klabu hiyo.
Timu zingine zilizofuzu nusu fainali ya kombe hilo ni, Sevilla, Valencia na Leganes.

0 comments:
Post a Comment